
Picha:tanzaniatoday.co.tz
Hakika wanawake wanaweza! Hongera
Mh Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuwa Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama
Cha Mapinduzi (CCM). Kuchaguliwa kwako kumeonyesha kuwa wanawake wanaweza
kuongoza ngazi yoyote ya uongozi nchini Tanzania. Jana jumapili ya tarehe 12
mwezi wa 07 mwaka 2015 mjini Dodoma ilikuwa siku ya kukumbukwa na watanzania na
hasa wakinamama nchini.
Kitendo hiki kimetoa hamasa kubwa
kwa wanawake wengi nchini Tanzania kujiamini kuwa wanaweza. Blogu hii inaomba
wanawake wazidi kujitokeza katika kuwania nafasi za maamuzi na kisiasa nchini
Tanzania kupitia uchaguzi mkuu utakaofanyia oktoba mwaka huu 2015.
Hakika wanawake wanaweza!
No comments:
Post a Comment