Monday, July 13, 2015

Hakika wanawake wanaweza! Hongera Balozi Amina na Dr Asha-Rose

Picha: un.org

Hakika wanawake wanaweza! Hongera Balozi Amina Salum Ali na Dr Asha-Rose Mtengeti Migiro kwa kuonyesha kuwa wanawake wanaweza. Kufika kwenu kwenye TATU BORA ya kutafuta mgombea urasi kwa tiketi ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumeonyesha kweli na kwa hakika wanawake nchini Tanzania wana uwezo mkubwa sana katika ngazi za maamuzi. Wakina mama hawa walifika tatu bora jumamosi tarehe 11/07/2015 mjini Dodoma pamoja na Mh John Pombe Magufuli.

Tendo mlilofanya limetoa hamasa kwa wanawake wengine nchini kujiamini. Ni matarajio ya blogu hii kuwa kwa kufuata nyayo za wakina mama hawa (Balozi Amina Salum Ali na Dr Asha-Rose Mtengeti Migiro), wanawake wengi sana nchini watajitokeza katika kuomba nafasi za udiwani, ubunge na uwakilishi kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2015. Blogu hii inaamini, ili taifa hili liwe na ustawi unaostahili wanawake wanapaswa kushiriki kikamilifu katika ngazi za maamuzi na kisiasa.

Ombi la blogu hii ni kwa wapiga kura wanawake na wanaume kuwapigia kura za ndio MAMA zetu. Hakika NANI KAMA MAMA. HAKUNA.....

Picha:cctv-africa

No comments:

Post a Comment