Thursday, November 19, 2015

Hongera Mh. Majaliwa kwa kupendekezwa na Rais kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Picha:pmoralg.go.tz

Hongera Mh. Kassim Majaliwa kwa kupendekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Blogu hii haina shaka na utendaji na uzoefu wako serikalini na hasa ulipokuwa TAMISEMI. Aidha blogu hii inatambua umakini, hekima, busara na upole ulionao. Kwa sasa blogu hii inakupongeza na kukutakia kila la kheri wakati Bunge likisubiriwa kukupitisha.

Wednesday, November 18, 2015

Hongera Mh Ndugai kwa kuchaguliwa kuwa Spika mpya wa Bunge la Tanzania 2015 - 2020

Picha: Habarileo.co.tz

Hongera Mh Job Ndugai kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa Spika mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha 2015 - 2020. Ushindi huo unathibitisha imani kubwa walionayo wabunge katika kusimamia chombo hiki muhimu kwa ustawi wa nchi yetu. Ni imani ya blogu hii utatimiza majukumu yako ikiwemo kuishauri na kuisimamia serikali ili Tanzania ipige hatua kubwa ya maendeleo. Hongera sana Mh Ndugai, Mwenyezi MUNGU akuongoze ili uliongoze Bunge hili kwa hekima, amani na upendo kwa kuzingatia kanuni, sheria na katiba.

Saturday, November 7, 2015

Tanzania isimamie AHADI 10 za mwana TANU kwa ukamilifu ili tupate taifa ADILIFU na lenye kuleta maendeleo kwa WOTE

Kwanza kabisa isieleweke vibaya kunukuu AHADI za mwana TANU. Blogu hii imeona AHADI za mwana TANU kama zikitumika nchi yetu itasonga mbele kwa kasi kubwa sana. TANU ni chama kilicholeta ukombozi toka kwa wakoloni. Kila mwananchi alipenda siasa hii chini ya usimamizi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa sababu ilijali utu wa binadamu, ilikuwa ikiwainua wanyonge na ililenga kulijenga Taifa katika misingi ya haki na usawa. Aidha mwananchi yoyote bila ya kujali hadhi yake alipotakiwa kujiunga na chama hizi ndizo ahadi kumi alizotakiwa kuzitekeleza kwa vitendo kinyume cha hapo hatua kali zinachukuliwa. Ahadi kumi za mwana TANU zilikuwa kama ifuatavyo:

  1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.
  2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote.
  3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.
  4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.
  5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
  6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.
  7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.
  8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
  9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika (sasa Tanzania) na Afrika.
  10. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanganyika (sasa Tanzania).

NAOMBA KILA MTU ASOME AHADI HIZI MWOYONI MWAKE NA AJIULIZE AMETEKELEZA NGAPI?

Blogu hii inamuomba rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania DKT John Pombe Joseph Magufuli na serikali yake atekeleze AHADI za mwana TANU. Blogu hii inatamani sana AHADI hizi zirudi na zitumike na kila mwana wa nchi hii bila kujali dini, kabila, elimu, kipato, chama, jinsi yake. Ahadi hizi zifundishwe toka shule za awali mpaka chuo kikuu ili tuzalishe taifa lenye UADILIFU uliotukuka. Naomba viongozi wote wa ngazi zote na hasa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ahakikishe AHADI hizi zinaimbwa na kila mtoto na mtu mzima wa taifa hili, zinatekelezwa na kila mtoto na mtu mzima wa taifa hili na pale zinapokiukwa HATUA kali zichukuliwe. Kwa kutizima AHADI hizi Tanzania itakuwa nchi bora sana. 

Thursday, November 5, 2015

Asante WATANZANIA kwa kudumisha AMANI wakati na baada ya UCHAGUZI

Picha:tanzaniatoday.co.tz

Asante WATANZANIA kwa kudumisha AMANI wakati na baada ya UCHAGUZI wa rais, wabunge na madiwani nchini Tanzania. Hakika Tanzania ni kisiwa cha AMANI. Blogu hii inawakumbusha watanzania wazidi kudumisha AMANI mara baada ya Rais wa AWAMU ya 5 kuapishwa. Blogu hii inasisitiza Mh. DKT. John Pombe MAGUFULI ni Rais wa WATANZANIA wote.

Hongera Mh MAGUFULI kwa kuapishwa na kuwa Rais wa TANZANIA

Picha:taarifa.co.tz

Hongera Mh. DKT. John Pombe MAGUFULI kwa kuapishwa na kuwa Rais wa awamu ya 5 ya Tanzania. Leo alhamisi tarehe 05 Novemba 2015 ni siku ya kukumbukwa na watanzania mara baada ya kuapishwa kama Rais wa Tanzania. Hakika watanzania wamekuamini na wanakutegemea katika kuwaletea maendeleo ya kweli. Ni matumaini ya Blogu hii kuwa utawaletea watanzania maendeleo kwa kasi kubwa. Blogu hii inaamini imepata mtetezi wa wanyonge. Mwenyezi MUNGU akubariki na kukulinda katika kuwatumikia wananchi wote.

Aidha Blogu hii inawaomba watanzania wote waunganishe NGUVU katika kuhakikisha ahadi za MAGUFULI na CCM zinatekelezwa kikamilifu. 

Hongera KIKWETE kwa kumaliza uongozi salama kama Rais

Picha: taarifa.co.tz

Hongera Mh. DKT. JAKAYA KIKWETE kwa kumaliza uongozi salama kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leo tarehe 05 Novemba 2015 katika uwanja wa UHURU jijini Dar es Salaam umemkabidhi kijiti cha uongozi Mh John Pombe Magufuli. Kwa kiasi kikubwa umejitahidi kuwatumikia wananchi. Blogu hii inasema ASANTE na upate mapunziko MEMA.