- Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.
- Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote.
- Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.
- Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.
- Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
- Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.
- Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.
- Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
- Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika (sasa Tanzania) na Afrika.
- Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanganyika (sasa Tanzania).
NAOMBA KILA MTU ASOME AHADI HIZI MWOYONI MWAKE NA AJIULIZE AMETEKELEZA NGAPI?
Blogu hii inamuomba rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania DKT John Pombe Joseph Magufuli na serikali yake atekeleze AHADI za mwana TANU. Blogu hii inatamani sana AHADI hizi zirudi na zitumike na kila mwana wa nchi hii bila kujali dini, kabila, elimu, kipato, chama, jinsi yake. Ahadi hizi zifundishwe toka shule za awali mpaka chuo kikuu ili tuzalishe taifa lenye UADILIFU uliotukuka. Naomba viongozi wote wa ngazi zote na hasa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ahakikishe AHADI hizi zinaimbwa na kila mtoto na mtu mzima wa taifa hili, zinatekelezwa na kila mtoto na mtu mzima wa taifa hili na pale zinapokiukwa HATUA kali zichukuliwe. Kwa kutizima AHADI hizi Tanzania itakuwa nchi bora sana.

No comments:
Post a Comment