Saturday, July 8, 2017

Hongera timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" kwa kuchukua nafasi ya 3 ya COSAFA

Tokeo la picha la tanzania flag
Picha: wikipedia

Hongera timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" kwa kushika nafasi ya 3 ya mashindano ya COSAFA nchini Afrika Kusini. Ushindi huo umekuja baada ya kuifunga Lesotho kwa mikwaju ya penati. Hakika wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa TFF chini ya Rais Jamal Malinzi mnastahili pongezi kwa hatua hii. Kipekee blogu hii inampongeza kocha Salum MAYANGA kwa kuiboresha timu ya Tanzania. Hakika, hivi sasa Tanzania inacheza soka zuri na la ushindani ukilinganisha na miaka ya nyuma. Hatua hii itainua Tanzania katika viwango wa FIFA na pia wachezaji watapata soko kimataifa. Aidha hatua hii imewafanya wachezaji kupata uzoefu na kuzoeana na hii itaiwezesha Tanzania kufanya vizuri katika michuano mingine ya kimataifa. 

Monday, June 12, 2017

Big UP kamati ya Profesa Osoro, "Raslimali za MADINI zitamkwe kuwa MALI ya WATANZANIA"

Tokeo la picha la Nehemiah Eliachim Osoro

Hongera kamati ya pili ya MAKINIKIA iliyoteuliwa na Mh Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa kuja na uchambuzi wa kina wa kiuchumi na kisheria. Kamati hii ya PILI chini ya uenyekiti wa Profesa Nehemiah Eliachim Osoro imefanya kazi nzuri kwa maslahi mapana ya taifa. Blogu hii inasema ASANTE. 

Blogu hii imefurahishwa na mapendekezo yote ya kamati ya PILI hasa "raslimali za MADINI zitamkwe kuwa MALI ya WATANZANIA".

Tokeo la picha la magufuli

Aidha blogu hii inampongeza Mh Rais kwa udhubutu wa kuamua masuala magumu ya kitaifa kwa maslahi ya taifa. Hakika, sasa Tanzania tunajivunia kuwa na kiongozi mtetezi na mlinzi wa raslimali zetu. Blogu hii inamuomba Mh Rais nguvu hii pia iende kwenye masuala mengine muhimu kama vile misitu, utalii, mikataba ya umeme, mikataba ya matumizi ya maji kwa ziwa Victoria nk ili watanzania wanufaike.

Tokeo la picha la KAMATI YA PILI YA MADINI WIKEPEDIA

 Picha: tanzaniatoday

Blogu hii inawaomba watanzania kuwa kitu kimoja katika harakati hizi za kutetea maslahi ya watanzania. Blogu hii inafahamu kuna kasoro ambazo zilijitokeza huko nyuma na kwa sasa serikali ya John Pombe MAGUFULI imedhamiria kuzifanyia kazi kikamilifu. Aidha blogu hii imefurahishwa na kauli ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Job Ndugai kwa kauli aliyoitoa ya kusaidiana na serikali kuzipitia na kurekebisha sheria za madini kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu. Blogu hii inasema ASANTE.


Tokeo la picha la job ndugai
Picha:ccm blog

Tuesday, June 6, 2017

Hongera Kamanda SIRRO kwa kuteuliwa kuwa IGP

Image may contain: 4 people, people smiling, people standing and outdoor
Hongera Kamanda SIRRO kwa kuteuliwa kuwa IGP. Hakika unastahili nafasi hii kutokana na utendaji wako na hasa ulipokuwa kamanda wa mkoa wa Dar es Salaam. Blogu hii inakuomba uchape kazi ili nchi iwe na amani na usalama zaidi. Aidha blogu hii inampongeza rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania DKT John Pombe Magufuli kwa kumteua kamanda SIRRO mchapakazi. 

Hongera mama Anna Mghwira kwa kuchaguliwa na rais kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro

Image may contain: 8 people, people smiling, people standing and suit

Hongera mama Anna Mghwira kwa kuchaguliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKT John Pombe Magufuli. Blogu hii inakutakia kila la kheri katika utendaji wako mpya wa Ukuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Ingizo lako katika serikali ni shule kwa watanzania wote, wenye vyama na wasio na vyama. Blogu hii inakuomba uwe mfano katika uwajibikaji kwa rais na kwa wananchi, hasa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro, uwe mwadilifu, mchapakazi na mtetea usawa kwa wote na hasa kwa kina mama na wanawake ambao bado katika nchi za kiafrika wanakabiliwa na changamoto nyingi. Aidha blogu hii inampongeza sana Mh Rais kwa uamuzi wake wa kumwamini mama ANNA ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa chama cha upinzani ACT Wazalendo. 

Wednesday, May 24, 2017

Hongera Rais MAGUFULI kwa kutetea rasilimali za Tanzania kupitia sekta ya madini

Tokeo la picha la magufuli
Picha: wikipedia

Hongera Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa kutetea rasilimali za Tanzania kupitia sekta ya madini. Blogu hii imefurahishwa na uamuzi wako wa kuteua Kamati Maalum ya kuchunguza mchanga wa mabaki ya madini ya dhahabu yanayosafirishwa nje ya nchi kupitia makontena. 

Kamati hiyo iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Profesa Abdukarim Hamis Mruma imefanya kazi nzuri kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Pia blogu hii inakupongeza kwa uamuzi wako wa leo wa kuwawajibisha wahusika na kuvunja bodi ya TMAA. Kwa mujibu wa ripoti inaonekana taifa letu linapoteza mapato makubwa kutokana na tofauti ya kiasi cha madini kinachosafirishwa kupitia makontena ya mabaki ya dhahabu na madini mengine.

Image may contain: 1 person, sitting

Aidha, blogu hii inaomba yafuatayo:
  • Watendaji wa serikali pamoja na taasisi zake ziwe makini na kufuatilia kwa karibu thamani halisi ya madini yanayochimbwa na pia kusafirishwa nje kupitia mchanga wa madini au madini halisi;
  • Ni vizuri taasisi kama TMAA, TRA, TBS na mamlaka za Bandari na viwanja vya ndege wafuatilie kwa umakini kiasi halisi cha madini kinachotoka nje ya nchi na kila taasisi ikiwezekana iwe na kumbukumbu zake;
  • Pia kuwepo na vifaa vya kiteknolojia vya kuchunguza kwa umakini makontena au mizigo inayopita bandarini na viwanja vya ndege;
  • Vyombo vya ulinzi na usalama vishiriki kikamilifu kulinda rasilimali za taifa na hasa kupitia katika mipaka ya nchi yetu;
  • Suala la MAADILI litiliwe mkazo kwa watumishi wote wa umma;
  • Taifa kupitia Wizara ya Nishati na Madini linunue kifaa cha kuchenjua madini "smelter" ili taifa liweze kupata faida ya rasilimali ya madini kwa uhalisia wake.

Kila la kheri Mh Rais Magufuli katika kulinda rasilimali za taifa. Watanzania tupo nyuma yako!

Sunday, May 21, 2017

Hongera Faidha Msangi kwa kushinda Urais wa Serikali ya Wanafunzi wa IAE

Tokeo la picha la institute of adult education
Hongera Faidha Msangi kwa kushinda Urais wa Serikali ya Wanafunzi wa Institute of Adult Education (IAE) mei 2017. Blogu hii imefurahishwa na ushindi wako ukiwa kama mwanamke shupavu. Ushindi wako umewaamsha wanawake na wanaume kuwa siku hizi na siku zijazo kuna fursa ya kila mwanamke na mwanamme kushinda ngazi yoyote ya uchaguzi bila tatizo lolote. 


Image may contain: 3 people, closeup
Uchaguzi huu unaweza kuonekana ni mdogo katika nchi yetu ila unatoa somo la kujifunza kwa jamii yetu ambayo imeathiriwa na mfumo dume. Blogu hii inaamini maendeleo ya kweli katika taasisi na jamii yoyote yatapatikana kwa kutoa nafasi sawa kwa wanawake na wanaume bila ubaguzi. 

Tokeo la picha la institute of adult education

Blogu hii inakuomba utumikie nafasi yako kwa weledi, ustadi na nguvu za hali ya juu ili jamii yetu izidi kupata imani kuwa mwanawake na mwanaume anaweza uongozi bila kujali jinsi. 


Blogu hii inaamini kama mwanamke anaweza kulea mtoto mpaka anakuwa mtu mzima basi bila shaka uwezo wa kuongoza taasisi au jamii upo ndani yake pia. Kila la kheri Faidha Msangi. Hakika wanawake WANAWEZA!

Sunday, May 14, 2017

Asante Mh Nyarandu, Samaritan's Purse na Serikali kwa kusaidia kuwapeleka watoto walionusurika na ajali Marekani kwa matibabu zaidi

Image may contain: 13 people, crowd, wedding and outdoor
Kwa hili la kusaidia kupeleka watoto watatu Marekani kwa ajili ya matibabu ni jambo la kupongezwa. Mh Lazaro Nyarandu, Mbunge wa Singida Kaskazini, Shirika la Kujitolea la Marekani Samaritan's Purse na Serikali ya Tanzania kwa hili mnastahili pongezi za dhati kabisa. 

No automatic alt text available.
Watoto hawa ni majeruhi wa ajali iliyopoteza uhai wa watoto, walimu na dereva wa shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha. Takribani zaidi ya watu thelathini walipoteza maisha wengi wao wakiwa wanafunzi wa darasa la saba waliokuwa wakielekea Karatu toka Arusha kwa ajili ya mitihani ya ujirani. 

Image may contain: outdoor
Blogu hii pia inawashukuru wafadhili (Samaritan's Purse) wa safari hii ya kwenda nchini marekani kwa matibabu zaidi. Aidha blogu hii inaishukuru Serikali ya Tanzania katika kufanikisha hili na kwa kukubali watoto hawa waende nje kwa matibabu zaidi.

Image may contain: sky, cloud and outdoor