
Hongera Faidha Msangi kwa kushinda Urais wa Serikali ya Wanafunzi wa Institute of Adult Education (IAE) mei 2017. Blogu hii imefurahishwa na ushindi wako ukiwa kama mwanamke shupavu. Ushindi wako umewaamsha wanawake na wanaume kuwa siku hizi na siku zijazo kuna fursa ya kila mwanamke na mwanamme kushinda ngazi yoyote ya uchaguzi bila tatizo lolote.

Uchaguzi huu unaweza kuonekana ni mdogo katika nchi yetu ila unatoa somo la kujifunza kwa jamii yetu ambayo imeathiriwa na mfumo dume. Blogu hii inaamini maendeleo ya kweli katika taasisi na jamii yoyote yatapatikana kwa kutoa nafasi sawa kwa wanawake na wanaume bila ubaguzi.

Blogu hii inakuomba utumikie nafasi yako kwa weledi, ustadi na nguvu za hali ya juu ili jamii yetu izidi kupata imani kuwa mwanawake na mwanaume anaweza uongozi bila kujali jinsi.

Blogu hii inaamini kama mwanamke anaweza kulea mtoto mpaka anakuwa mtu mzima basi bila shaka uwezo wa kuongoza taasisi au jamii upo ndani yake pia. Kila la kheri Faidha Msangi. Hakika wanawake WANAWEZA!
No comments:
Post a Comment