
Jana Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania lilipitisha bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa fedha 2017/18. Blogu hii inampongeza Waziri Mh Ummy Mwalimu kwa hotuba yake nzuri iliyowafanya wabunge wapitishe bajeti hiyo. Blogu hii inajua umuhimu wa huduma za afya nchini na hivyo ahadi zote zilizotolewa na kupangwa na Wizara zikitekelezwa kikamilifu hasa kuokoa vifo kwa wanawake wajawazito na watoto.

Blogu hii inafahamu kuwa Wizara hii ina mambo mengi sana ya kuyatekeleza kwa maana wa ukubwa na majukumu yake. Blogu hii inaomba watumishi na watendaji wa sekta ya afya na Wizara kwa ujumla kuimarisha huduma za afya nchini.
Aidha blogu hii inaomba serikali iweke na kutangaza utaratibu wa kutoa huduma kwa wazee hasa za afya na matibabu. Blogu hii inaamini kuwa kuna utaratibu wa kuwahudumia wazee lakini kuna haja kuwe na utaratibu wa kuwajulisha watanzania juu ya huduma fulani fulani kwa wazee kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Blogu hii inajua wazee hukosa nguvu na fedha za kujihudumia kiafya wakiwa na umri mkubwa.
No comments:
Post a Comment