
Hongera Dr Fatma Hamad mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa la jinsia "1st International Conference on Gender Issues in Higher Learning Institution".
Hakika blogu hii inakupongeza kwa umahili na ustadi wako uliowezesha kongamano hili. Aidha blogu hii inawapongeza wajumbe wa kamati ya maandalizi wote pamoja na uongozi mzima wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam.
Blogu hii inatarajia kuona makongamano mengine mengi katika chuo hiki yenye kuchochea maendeleo ya taaluma na nchi yetu.
Blogu hii inaomba mapendekezo aliyoyatoa mgeni wa heshima Mh Ummy Mwalimu kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan yafanyiwe kazi, hasa suala la kufanya utafiti juu ya suala la elimu bure na ongezeko la wanafunzi wa kike na kiume nchini.



No comments:
Post a Comment