
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama
Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakandarasi wa ndani jana (04 MEI 2017) amesema
serikali itawapa kipaumbele wakandarasi wa ndani. Hakika tamko hili
limekuja wakati muafaka ambapo itainua kipato cha wakandarasi wa ndani na
kuinua uchumi wa nchi.
Blogu hii inaomba wakandarasi wa ndani wafanye mambo yafuatayo:
- Kufanya kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa;
- Kukamilisha kandarasi kwa viwango kwa mujibu wa mikataba;
- Kukamilisha kandarasi kwa wakati na kwa mujibu wa mikataba;
- Kujiunga pamoja na kushirikiana katika kazi ili kushindana na wakandarasi wa nje wenye nguvu.

Aidha, blogu hii inaiomba serikali kuweka sera ambazo
zitawawezesha makandarasi wa ndani kupata kiurahisi mikopo ya vifaa na kifedha.
No comments:
Post a Comment