
Watanzania tutembelee MIKUMI ili kukuza utalii wa ndani. Mikumi National Park ni mojawapo ya vivutio vizuri vya utalii Tanzania vyenye wanyama wengi wa porini.

Hivyo blogu hii inawahimiza watanzania watembelee mbuga hii kwa ajili ya kupunzika, kujifurahisha na kujifunza tabia mbalimbali za wanyama wa porini. Aidha blogu hii inaipongeza MIKUMI na TANAPA kwa ujumla kwa kuendeleza na kuimarisha utalii.

Ni vyema MIKUMI na TANAPA kwa ujumla ikawahamasisha watanzania kutembelea mbuga zetu na kuinua pato la taifa. Blogu hii inaomba kufanyike maboresho hasa MIKUMI kwenye njia za mbugani hasa wakati wa vipindi vya mvua.

Blogu hii inajua mbuga za wanyama hazitakiwi ziwe na barabara za lami lakini wanaweza kuweka barabara za changarawe ili njia zipitike kwa urahisi na hasa kwenye vipindi vya mvua. Pia huduma za kulala na chakula ziimarishwe na ziwe kwenye viwango vya kimataifa ili kuwavutia watalii wa ndani na nje.

No comments:
Post a Comment