
Kwa hili la kusaidia kupeleka watoto watatu Marekani kwa ajili ya matibabu ni jambo la kupongezwa. Mh Lazaro Nyarandu, Mbunge wa Singida Kaskazini, Shirika la Kujitolea la Marekani Samaritan's Purse na Serikali ya Tanzania kwa hili mnastahili pongezi za dhati kabisa.

Watoto hawa ni majeruhi wa ajali iliyopoteza uhai wa watoto, walimu na dereva wa shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha. Takribani zaidi ya watu thelathini walipoteza maisha wengi wao wakiwa wanafunzi wa darasa la saba waliokuwa wakielekea Karatu toka Arusha kwa ajili ya mitihani ya ujirani.

Blogu hii pia inawashukuru wafadhili (Samaritan's Purse) wa safari hii ya kwenda nchini marekani kwa matibabu zaidi. Aidha blogu hii inaishukuru Serikali ya Tanzania katika kufanikisha hili na kwa kukubali watoto hawa waende nje kwa matibabu zaidi.

No comments:
Post a Comment