Hongera Bi Jane Magigita kwa kutunukiwa tuzo ya haki ya mwaka 2014 ya Dr Martin Luther King baada ya mchango wako wa kutetea haki za kisheria za wanawake kutambuliwa. Kwa sasa Bi Jane ni mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali iitwayo "Equality for Growth". Bi Jane ametunukiwa tuzo hiyo na kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Virginia Blaser.
Bi Jane ametunukiwa tuzo hiyo kwa juhudi zake za kutetea haki za wanawake hususan katika kupinga ukatili wa kijinsia, matatizo ya urithi na matumizi ya ardhi.
Blogu hii inampongeza sana Bi Jane kwa kupata tuzo hii. Tuzo hii imeifanya dunia kutambua mchango wake kwa kuwasaidia wanawake maskini nchini Tanzania. Tuzo hii pia imeifungua Tanzania katika uso wa dunia kuwa ni nchi inayokabiliana na unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.
Blogu hii inamuomba Bi Jane aendelee katika juhudi zake za kuwapigania wanawake nchini Tanzania. Wanawake ni dada, mama na bibi zetu na ni lazima sote tuwapiganie kwakuwa wametutoa mbali katika maisha ya kila mmoja wetu. Pia wanawake kama walivyo wanaume wanastahili haki sawa. Hongera sana Bi Jane Magigita na MUNGU akutie NGUVU zaidi. Kwa habari zaidi soma Habari leo
No comments:
Post a Comment