Hongera Rose Ndauka kwa kuanzisha kampeni ya usafi nchini Tanzania. Rose Ndauka ni msanii wa filamu nchini Tanzania. Hivi karibuni Rose akiwa na wasanii wenzake walifanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Mnazi Mmoja
ndani ya jiji la Dar es Salaam. Aidha msanii huyo amezindua kampeni ya usafi iitwayo 'Amka
Badilika, Nga'risha Tanzania'.
Hakika blogu hii imefurahishwa na kitendo cha kuanzisha kampeni ya usafi nchini pamoja na kufanya usafi kivitendo.
Jiji la Dar es Salaam pamoja na majiji na halmashauri zingine nchini zinakabiliwa na changamoto ya usafi. Jukumu la kuhakikisha usafi katika majiji ama manispaa ama halmashauri liko mikononi mwa taasisi husika pamoja na wadau wengine wakiwemo wananchi kama msanii Rose Ndauka alivyofanya.
Blogu hii inaomba majiji, manispaa na halamashauri nchini zimpe Rose ushirikiano unaostahili katika kufanikisha azma yake ya usafi. Pia ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira itoe ushirikiano wa dhati juu ya juhudi zozote zinazofanywa na wadau kama Rose Ndauka.
Vile vile blogu hii inaomba majiji, manispaa na halmashauri zihakikishe maeneo yao yanakuwa safi muda wote. Kuyafanya majiji ama manispaa ama halmashauri kuwa safi ni jambo linalowezekana. Taasisi hizi zinapaswa kutenga fedha za kodi kwa kiasi fulani ili kuhakikisha maeneo yote yanakuwa safi. Pia kuna by-laws ambazo majiji ama manispaa kupitia kata husika wanaweza kuzitekeleza ili kulazimisha watu na jamii zifuate kanuni ya usafi. Mfano mtu akitupa taka ovyo hata kama ni ganda la embe by-laws ziko wazi achukuliwe hatua papo hapo. Vile vile katika maeneo ama nyumba za watu ama vituo vya daladala kuwe na vyombo vya uchafu ili watu waweze kutupa taka taka. Magari ya abiria kama dala dala yawe masafi na kuwa na vyombo vya kuhifadhia uchafu.
Pia askari mgambo wa majiji, manispaa ama halmashauri wapewe mafunzo mazuri ili kusimamia zoezi la usafi nchini Tanzania.
Taasisi husika kama vile majiji, manispaa na halmashauri zinaweza pia kuanzisha miradi ya kutumia taka kuzalisha gesi ama umeme. Na pia taka zingine zinaweza kubadilishwa na kutumiwa tena kama bidhaa. Baadhi ya nchi kwa mfano wanatumia taka kuzalisha umeme ambao unaingizwa kwenye gridi ili kuwapa wananchi wake umeme. Hivyo blogu hii inaamini usafi ni jambo linalowezekana na pia ni sekta ambayo ikitumiwa vizuri itaajiri vijana wengi na kutoa faida zingine kama vile gesi na umeme. Ni jukumu la taasisi husika zikafanyia kazi masuala haya ili kufanikisha usafi katika mazingira yetu.
Falsafa ambayo mdau wa blogu hii aliipata nje ya nchi hii ni kuwa ukitaka kufanikisha usafi katika eneo lolote ni lazima "utumie uchafu kama fursa". Nini maana yake? Uchafu upo! Ila unatakiwa kuratibiwa. Mfano mabaki ya chakula yakikusanywa toka majumbani yanaweza kutumika kutoa gesi ama mbolea.Gesi ama mbolea itokanayo na taka inaleta faida kwenye uchumi wa nchi na mtu moja mmoja pia.

Blogu hii inaamini USAFI nchini UNAWEZEKANA kama WADAU wote kwa ujumla watashirikiana kikamilifu.
Kwa habari zaidi na picha bofya hapa.
Picha: http://pro-24.blogspot.com

Rose Ndauka akiwa na Meya wa Ilala, Jerry Slaa pamoja na wanafunzi na wasanii wenzake wakifanya usafi katika eneo la Mnazi Mmoja
ikiwa ni kampeni ya kufanya usafi jiji zima la Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment