Hongera kampuni ya simu ya Tigo kwa kutoa msaada wa vitabu vya wanafunzi wa
darasa la saba na nne katika Shule ya Msingi Kilimani wenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni sita. Aidha, meneja wa Huduma za Kijamii kutoka Tigo, Woinde
Shisael alisisitiza kuwa kampuni hiyo ya Tigo inatambua umuhimu wa elimu kama
mojawapo ya kiungo katika kuchangia mabadiliko ndani ya jamii ama Taifa. Hakika, huo ni ukweli mtupu.
Vile vile kwa kupitia wafanyakazi wa Tigo shule hiyo ilikabidhiwa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita takribani elfu nne za maji. Tenki hilo lina thamani ya shilingi za kitanzania laki sita na elfu hamsini na tatu.
Hakika blogu hii imefurahishwa na juhudi za kampuni hii ya simu za mkononi kwa kutambua mchango wa elimu katika taifa letu. Pia blogu hii imefurahishwa na wafanyakazi wa kampuni hii ya simu ya Tigo kwa kutoa msaada muhimu wa tenki la maji kwa shule hiyo. Blogu hii inawaomba Tigo kuendelea kuwasaidia watanzania kwa njia mbali mbali na hasa kwa kupitia sekta ya elimu. Elimu ni kila kitu kwa binadamu yoyoye. Waswahili wanasema "elimu ni ufunguo wa maisha". Hivyo kwa Tigo kutoa mchango wa aina hiyo wameweza kuchochea maendeleo ya elimu nchini. Asante Tigo!
Blogu hii imeona ni vyema kuwaunganisha wadau wake na Tigo kama ni namna mojawapo ya kukubali juhudi zao kwa watanzania!
Aidha blogu hii inayaomba makampuni mengine kuiga mfano mzuri wa Tigo katika kuchangia maendeleo ya nchi na wananchi hasa kupitia sekta ya elimu. Kwa habari zaidi bofya hapa.
Picha:en.wikipedia.org
No comments:
Post a Comment