Wazo la kuwa na mfumo wa bei elekezi wa ada kwa shule za msingi na sekondari ni zuri sana. Wazo hilo limesemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dr Shukuru Kawambwa wakati alipokuwa akizindua mfumo wa ada elekezi kwa vyuo vya Elimu ya Juu nchini.
Hakika, blogu hii imefurahishwa na hatua hiyo ya serikali kwa kuwa itaboresha sekta ya elimu nchini. Bei elekezi ya ada inakokotolewa kitaalamu kwa kuweka gharama zote za uendeshaji chuo ama shule. Hii itatoa unafuu kwa wazazi ama taasisi zinazofadhili wanafunzi kwa maana ya kuwa na gharama za ukweli hata kama zitakuwa juu. Hii itapelekea ubora wa elimu kuongezeka kwa maana kama ada itajumuisha matumizi ya maabara na kemikali katika ufundishaji kivitendo basi mwanafunzi atatarajiwa kupata elimu ya kiwango hicho na siyo vinginevyo.
Kuhusu wazo la kuwa na ada elekezi kwa shule za msingi na sekondari ni kuwa suala hili ni la msingi sana. Baadhi ya shule za msingi nchini kwetu zimekuwa na kasumba ya kupandisha ada kiholela kwa sababu zisizo za kitaalamu. Zipo shule za msingi ambapo ada kwa mwaka kwa mwanafunzi mmoja inazidi ada ya mwanafunzi kwa ngazi ya shahada ama stashahada kwa baadhi vyuo nchini. Hii HAIKUBALIKI! na sio KWELI!
Mbali na kuipongeza serikali kwa kuwa na wazo zuri sana la kuwa na ada elekezi, Blogu hii inaishauri serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuanzisha taasisi ama "agency" ya serikali itakayosimamia viwango hivi vya ada elekezi. Kwa maneno mengine kuwe na "regulator" ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora kulingana na ada inayolipwa. Bila ya kuwa na "regulator" suala hili licha ya kuwa zuri utekelezaji wake utakuwa na walakini. Taasisi hii itakayoanzishwa inaweza pia hata kuhusika na masuala ya UKAGUZI wa shule ili Wizara ibaki kama msimamizi mkuu wa elimu kisera.
Waziri wa Elimu Dr Shukuru Kawambwa wakati wa uzinduzi wa kituo kiitwacho "Teachers
Professional Center" DUCE tarehe 23 oktoba 2013. Katikati ni Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Gharib Bilal
No comments:
Post a Comment