Wednesday, September 7, 2016

Hongera JPM kwa kuhimiza ujenzi wa haraka wa nyumba za kisasa Magomeni Kota



Hakika, uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kutaka ujenzi wa nyumba za kisasa kwenye viwanja vya magomeni kota (Quarters) kuanza ni wa kuungwa mkono na kila mwananchi wa nchi yetu. Hakika ujenzi huu umekaa kwa muda mrefu bila kuanza.

Blogu hii inampongeza sana Rais JPM kwa kuwahimiza wahusika wa mradi huu kuanza ujenzi. Miaka mitano iliyopita Manispaa ya Kinondoni iliwaondoa wakazi katika eneo hilo na kubomoa nyumba zao kwa ahadi ya kujenga nyumba za kisasa. Lakini mpaka sasa hakuna ujenzi wowote ulioanza. 

Aidha kuna maeneo mengi ya miradi ambayo kwa sababu zisizojulikana ujenzi wake haujaanza. Mfano mzuri ni mradi wa majengo pale karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, maeneo karibu na Mchikichini yakitizamana na Msimbazi Center.

Blogu hii inaomba miradi hiyo ya ujenzi iweze kuanza ili mbali ya jiji la Dar es Salaam kupata mandhari nzuri pia wakazi wengi wa Dar es Salaam watapata makazi bora. Blogu hii inakumbusha, miaka mingi iliyopita Rais wa Zanzibar wakati ule Karume (senior) aliweza kusimamia ujenzi wa majengo mengi na makubwa na imara na mpaka sasa Zanzibar inajivunia hilo. Sasa hata wakati huu tulionao tunaweza ni kudhubutu na kuchukia hatua.



Monday, August 8, 2016

Tumuunge mkono JPM kuamia Dodoma

Picha:en.wikipedia.org
Hakika, uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa serikali yake kuamia Dodoma ni wa kuungwa mkono na kupongezwa. Rais John Pombe Magufuli alitoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti julai mwaka huu.

Blogu hii inaupongeza na kuunga mkono uamuzi huu na inawaomba watanzania wote kuunga mkono ili malengo yaliyowekwa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Nyerere miaka ya sabini yaweze kutimia.

Kijiografia, Dodoma ni katikati ya Tanzania na ni rahisi kufikika toka kona mbalimbali za nchi. Pia kiusalama, Dodoma ni mahali salama kwa nchi. Kiuchumi, Dodoma ni kiunganishi cha mikoa mingine nchini.

Blogu hii inaomba vyombo vyote vya serikali kujipanga na kutengeneza mikakati ya muda mfupi, wa kati na mrefu (sio zaidi ya miaka mitano) kuhakikisha Dodoma inakuwa makao makuu kwa vitendo kiutawala, kisiasa, kiuchumi na kimiundombinu.

Blogu hii pia inaomba mamlaka za mkoa wa Dodoma na hasa CDA kujiongeza zaidi kwa kutengeneza miundombinu inayolenga mahitaji ya sasa na miaka 100 ijayo. Blogu hii ingependa hata kama uwezo wa kutengeneza barabara za lami zenye njia zaidi ya nane kwa pamoja haupo basi kwa makusudi ni muhimu kuacha sehemu ya barabara kwa ajili hiyo. Pia kubakisha sehemu ya upanuzi wa majengo ya serikali kama viwanja vya ndege, vituo vya reli, vituo vya mabasi, vituo vya maroli, hospitali, shule, vyuo nk ili upanuzi uweze kufanyika bila ya serikali kuingia kwenye ghrama kubwa ya kulipa fidia.

Mwisho, CDA na mamlaka za kiutawala Dodoma ziweke au ziuishe mpango wa mji wa Dodoma kwa kuwa na sehemu maalumu za viwanda vikubwa na vidogo (visiingiliwe), masoko makubwa ya kisasa (yenye kuzingatia usafi na mazingira), makazi bora ya watu yaliyo na mpangilio sawa (kama ni sehemu inatakiwa ghorofa moja mpaka nne basi ziwe hivyo au sehemu ni ghorofa kumi na kuendelea iwe hivyo hivyo).

Thursday, June 30, 2016

Tumuunge mkono JPM kwa kulipa kodi...ukiuza toa risiti...ukinunua dai risiti...

Tokeo la picha la magufuli
Picha:cctv-africa.com
Tumuunge mkono JPM kwa kuhakikisha kila mtanzania analipa kodi. Rais John Pombe Magufuli amejipambanua katika kuwaletea wananchi maendeleo. Katika juhudi zake hizo amewahimiza sana wananchi na hasa wafanyabiashara kulipa KODI. Nchi zote zilizopiga hatua kubwa ya maendeleo zinahakikisha kila mwananchi analipa kodi inayostahili. 

Blogu hii imependa kauli ya Mh Rais isemayo "...ukiuza toa risiti....ukinunua dai risiti..." ili kodi irudi serikalini kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi.

Aidha blogu hii inaomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya kodi kikamilifu na kuwashughulikia wale wote wanaokwepa kukwepa kodi. Aidha blogu hii inaishauri serikali kutafuta vyanzo vipya vya kupata mapato ambavyo havijaguswa.

....UKIUZA TOA RISITI....UKINUNUA DAI RISITI.....

Wednesday, April 20, 2016

Hongera Serengeti Boys kwa kuwafunga mafarao wa Misri mara mbili

Picha: tanzaniatoday.com
Licha ya kuwa ilikuwa mechi ya kirafiki ya kimataifa, blogu hii inaipongeza timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 serengeti boys kwa kuifunga timu ya taifa ya Misri mara mbili. Hakika kila mtanzania anajua ubora wa timu za Misri na hivyo kiwango walichoonyesha vijana wetu wa kitanzania kinahitaji pongezi za dhati. Pia blogu hii inawapongeza makocha na benchi zima la ufundi kwa juhudu walizofanya na wanazoendelea kufanya. Pia tunaipongeza TFF kwa kuilea timu hii na kuwa na mafanikio haya. Blogu hii inaomba TFF na wadau wengine wa mpira wa miguu nchini na hasa wizara ya Elimu, Michezo na TAMISEMI kuunganisha nguvu na kuwa na mpango wa kuhakikisha michezo inachezwa na kushindaniwa kwenye shule zetu kiwilaya, kimkoa, kikanda na kitaifa. Kwa kufanya hivyo taifa litaweza kuwa na vijana wengi wenye vipaji na wanaojitambua maana watakuwa na ujuzi wa michezo na elimu ya darasani pia.

Hongera Dr John Pombe Magufuli kwa kuzindua daraja la kigamboni

Picha: teamtz.com
Hongera Dr John Pombe Magufuli kwa kuzindua daraja la kigamboni jana tarehe 19 Aprili 2016. Blogu hii inakupongeza wewe binafsi kwa kuwa ndiye ulikuwa waziri wa ujenzi wakati mchakato wa ujenzi unaendelea. Hakika daraja hili ambalo umependekeza liitwe daraja la nyerere linakuwa kioo cha taifa na pia litachochea maendeleo eneo la kigamboni na Dar es Salaam kwa ujumla. Pia tunaipongeza shirika la hifadhi ya jamii NSSF chini ya uongozi wa aliyekuwa mtendaji mkuu wake aliyepita Dr Ramadhan Dau kwa kutoa baadhi ya fedha zilizowezesha ujenzi wa daraja hili. Pia blogu hii inaipongeza serikali ya Jakaya Kikwete kwa kutoa uamuzi wa ujenzi wa daraja hili.

Blogu hii inaomba daraja hili litunzwe na watu wote na wasimamizi wawe wakali kwa yeyote atakayehujumu miundombinu ya daraja hili. Blogu hii inasema hivi kutokana na baadhi ya watu wasiowaaminifu kuhujumu miundombinu ya barabara na madaraja kwa sababu mbalimbali kama uuzaji wa vyuma chakavu. 

Aidha blogu hii inaomba serikali kuendelea na juhudu ya ujenzi wa barabara na hasa za juu jijini Dar es Salaam na majiji mengine ili kuondoa kero ya msongamano wa magari. 

Sunday, February 28, 2016

Hongera Mh Paul Makonda kwa kuwawezesha walimu kutolipa nauli za daladala jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 07 2016

Picha:taarifa.co.tz
Hongera Mh Paul Makonda Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kufanikisha jambo zuri sana la walimu jijini Dar es Salaam kusafiri bure ndani ya daladala. Kuanzia tarehe 07 Machi 2016 walimu wote wa shule za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam hawatalipa nauli za daladala. Hakika blogu hii imefurahishwa sana na kiongozi huyu kijana ambaye amefanya jambo zuri nchini. Blogu hii inawapongeza pia viongozi wa wenye mabasi ya daladala kwa kukubaliana na wazo la Mkuu wa Wilaya. Hakika walimu ni watu muhimu sana katika taifa lolote, hususan Tanzania. Blogu hii inaomba viongozi wengine waige ubunifu kama wa Mkuu huyu wa Wilaya ya Kinondoni.

Sunday, January 10, 2016

Hongera Samata kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa Afrika kwa wachezaji wa ndani 2015

Picha: taarifa.co.tz

Hongera Mbwana Samatta kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa barani Afrika kwa wachezaji wa ndani 2015. Hakika umeitangaza Tanzania kwenye ramani ya dunia. Blogu hii inakupongeza sana na kukutakia mafanikio mema. Blogu hii inawapongeza wadau wote waliofanikisha mafanikio ya Samatta kwa namna moja ama nyingine hasa Mh Ismail Aden Rage akiwa Rais wa Simba kwa wakati huo kwa kumruhusu kijana huyu kwenda TP Mazembe kucheza soka la kulipwa. Pia blogu hii inazishukuru klabu ya Simba Sports na African Lyon ya Mbagara kwa kumtunza na kumwonyesha njia kijana huyu. Aidha blogu hii inaishukuru TFF pamoja na Wizara ya Habari, Michezo na Wasanii na hasa Waziri wake Mh Nape Nnauye kwa jinsi alivyoonyesha ukaribu katika masuala muhimu ya soka na hasa suala la Samatta. 

Aidha blogu hii inawapa changamoto wachezaji wengine wa Tanzania na hasa wenye umri mdogo kufuata nyayo za Mbwana Samatta ili waweze kufikia malengo makubwa na kuwa wachezaji wakubwa wa kulipwa duniani.

Pia blogu hii inawaomba wadau wa soka nchini kuhakikisha wanajenga miundombinu sahihi ya kuibua vijana kama Samatta na hasa TFF kuhakikisha inaratibu uwepo wa "soccer academy" nyingi nchini kwa kushirikiana na serikali kupitia wizara za Michezo, Elimu na Tamisemi. Pia kuna haja ya serikali kuteua shule maalum za michezo na hasa soka na pia kuwa na vyuo vya ualimu vinavyozalisha wakufunzi wa michezo. Pia Wizara ya Elimu iweke somo la michezo na hasa kwa vitendo katika mtaala na katika mashule yote nchini ili kila mwanafunzi wa ngazi ya chini mpaka juu acheze na kujua angalau mchezo mmoja na hii itajenga utamaduni mzuri nchini. Pia serikali inaweza kutoa "incentive" kwa wanafunzi wenye kuonyesha kipaji cha mchezo wowote kwa kuhakikisha mwanafunzi huyo anafikia malengo. Pia ni wakati kwa jamii na serikali kwa ujumla kutambua nafasi ya michezo na usanii kama sehemu ya shughuli inayoweza kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.