Mh.
Ummy Mwalimu (Naibu Waziri) akiwa katika kikao cha “8th African Roundtable on Sustainable Consumption and Production” Windhoek, Namibia. Mh. Ummy ameshiriki kikao hiki kwa niaba ya Mawaziri wa
Mazingira wa Afrika. Ikumbukwe, Tanzania ni Rais wa Mkutano wa Mawaziri wa
Mazingira wa Africa (African Ministerial
Conference on Environment - AMCEN). Katika kikao hiki alichohudhuria Mh. Ummy suala la kukuza uchumi na kupunguza umasikini Barani Afrika bila kuharibu mazingira pamoja na suala zima la "sustainable development" katika uzalishaji "comsumption/production" vimetiliwa mkazo.
Blogu hii imefurahishwa na madhumuni ya mpango wa
kushirikisha wadau mbalimbali katika mipango ya kukuza uchumi na kupunguza
umasikini Barani Afrika bila kuharibu mazingira kupitia kikao hiki
anachohudhuria Mh. Ummy.
Hapa nchini kwetu Tanzania kuna mipango mingi sana ya
kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Kauli hii ya kukuza uchumi na kupunguza
umasikini bila kuharibu mazingira ni nzuri sana na ndiyo kwa sasa inatakiwa kupewa
kipaumbele. Kauli hii inatakiwa iwekwe kwenye mipango mbalimbali nchini. Ni
vyema ikajulikana kuwa “sustainable development” siyo mpango mmoja BALI ni dhana
“mtambuka” haswa. Kwa maana katika mipango yetu iwe ya uzalishaji ama mingineyo lazima izingatie suala zima la “sustainable
development” kwa maana ya utunzaji wa mazingira, uwiano wa raslimali kwa watu
wote pamoja na kujali vizazi vijavyo.
Hili la kujali vizazi vijavyo katika mipango yetu ni muhimu
sana kwa maana raslimali zinazovunwa kuna siku zitakwisha wakati kizazi cha leo
kitakuwa HAKIPO duniani. Na vizazi vyetu wakati huo vitaona sisi watu wa leo
hatukutenda haki kwao.
Nchi kama Sweden wana “sustainable development” katika
sekta mbalimbali, mojawapo ya sababu wanayotaja kwa nini wanazingatia suala hili
katika sekta hizo za uzalishaji mali ni kuokoa vizazi vijavyo mbali ya kutunza
mazingira pekee. Mfano mmoja wapo wanaotoa ni kuwa kama viwanda vitazalisha
mali huku vikichafua anga ya juu kupitia moshi wenye kemikali basi “anga” itaharibika
na miale hatari ya jua itawaathiri binadamu ambao sio
SISI WA SASA! Hapa Tanzania pia tunapaswa kutilia mkazo dhana za wenzetu
kwani dunia ni moja ukiiangalia kwa jicho la tatu.
Pia blogu hii imefurahishwa na namna Mh Ummy anavyofikiria
kukutana na wadau kama CTI hapa nchini katika kuhakikisha uzalishaji endelevu unakuwa
kama kigezo cha kuchagua washindi wa “Tuzo
ya Rais ya mzalishaji Bora” itolewayo kila mwaka. Blogu hii inaomba CTI,
NEMC pamoja na wadau wengine
(ambao ni wengi kama vile viwanda, wakulima wenye mashamba makubwa na madogo,
wafugaji nk) kuhakikisha katika mipango yao wanazingatia dhana ya “sustainable
development” kwa maana ya kutunza mazingira, kujali vizazi vijavyo na kuzingatia
usawa katika raslimali.
Mwisho, blogu hii inapenda kutoa nini maana ya “usawa katika
raslimali na kujali vizazi vijavyo”. Mfano mzuri ni namna Rais wa Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania alivyokuwa akielezea namna raslimali ya gesi itakavyotoa
mchango mkubwa katika uchumi wetu LAKINI pia pasipo kutumia faida yake yote
katika kizazi hiki kupita kiasi bila kuangalia kizazi kingine kijacho. Kwa
maana raslimali iliyopo licha ya kuoa faida kubwa kiuchumi kuna siku itakwisha!
Je, sisi wa kizazi hiki ndio tuna haki pekee ya faida ya raslimali kama gesi
toka Mtwara? HAPANA! Lazima tuungane na Rais JK pamoja na Mh. Ummy katika suala
la "sustainable development" katika kila sekta ya uzalishaji nchini.



Safi sana Mh Ummy kwa kuwajali watanzania. sustainable development ndio mpango mzima
ReplyDeleteMipango endelevu ndio itiliwe mkazo hapa Tanzania ili kutunza mazingira na kulinda vizazi vijavyo
ReplyDelete