Wednesday, May 14, 2014

Asante Mh. Ummy Mwalimu kwa kuwakumbusha watanzania suala la "sustainable development"

Mh. Ummy Mwalimu (Naibu Waziri) akiwa katika kikao cha “8th African Roundtable on Sustainable Consumption and Production” Windhoek, Namibia. Mh. Ummy ameshiriki kikao hiki kwa niaba ya Mawaziri wa Mazingira wa Afrika. Ikumbukwe, Tanzania ni Rais wa Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira wa Africa (African Ministerial Conference on Environment - AMCEN). Katika kikao hiki alichohudhuria Mh. Ummy suala la kukuza uchumi na kupunguza umasikini Barani Afrika bila kuharibu mazingira pamoja na suala zima la "sustainable development" katika uzalishaji "comsumption/production" vimetiliwa mkazo.

Blogu hii imefurahishwa na madhumuni ya mpango wa kushirikisha wadau mbalimbali katika mipango ya kukuza uchumi na kupunguza umasikini Barani Afrika bila kuharibu mazingira kupitia kikao hiki anachohudhuria Mh. Ummy.

Hapa nchini kwetu Tanzania kuna mipango mingi sana ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Kauli hii ya kukuza uchumi na kupunguza umasikini bila kuharibu mazingira ni nzuri sana na ndiyo kwa sasa inatakiwa kupewa kipaumbele. Kauli hii inatakiwa iwekwe kwenye mipango mbalimbali nchini. Ni vyema ikajulikana kuwa “sustainable development” siyo mpango mmoja BALI ni dhana “mtambuka” haswa. Kwa maana katika mipango yetu iwe ya uzalishaji ama mingineyo lazima izingatie suala zima la “sustainable development” kwa maana ya utunzaji wa mazingira, uwiano wa raslimali kwa watu wote pamoja na kujali vizazi vijavyo.

Hili la kujali vizazi vijavyo katika mipango yetu ni muhimu sana kwa maana raslimali zinazovunwa kuna siku zitakwisha wakati kizazi cha leo kitakuwa HAKIPO duniani. Na vizazi vyetu wakati huo vitaona sisi watu wa leo hatukutenda haki kwao.

Nchi kama Sweden wana “sustainable development” katika sekta mbalimbali, mojawapo ya sababu wanayotaja kwa nini wanazingatia suala hili katika sekta hizo za uzalishaji mali ni kuokoa vizazi vijavyo mbali ya kutunza mazingira pekee. Mfano mmoja wapo wanaotoa ni kuwa kama viwanda vitazalisha mali huku vikichafua anga ya juu kupitia moshi wenye kemikali basi “anga” itaharibika na miale hatari ya jua itawaathiri binadamu ambao sio SISI WA SASA! Hapa Tanzania pia tunapaswa kutilia mkazo dhana za wenzetu kwani dunia ni moja ukiiangalia kwa jicho la tatu.

Pia blogu hii imefurahishwa na namna Mh Ummy anavyofikiria kukutana na wadau kama CTI hapa nchini katika kuhakikisha uzalishaji endelevu unakuwa kama kigezo cha kuchagua washindi wa “Tuzo ya Rais ya mzalishaji Bora” itolewayo kila mwaka. Blogu hii inaomba CTI, NEMC pamoja na wadau wengine (ambao ni wengi kama vile viwanda, wakulima wenye mashamba makubwa na madogo, wafugaji nk) kuhakikisha katika mipango yao wanazingatia dhana ya “sustainable development” kwa maana ya kutunza mazingira, kujali vizazi vijavyo na kuzingatia usawa katika raslimali.

Mwisho, blogu hii inapenda kutoa nini maana ya “usawa katika raslimali na kujali vizazi vijavyo”. Mfano mzuri ni namna Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania alivyokuwa akielezea namna raslimali ya gesi itakavyotoa mchango mkubwa katika uchumi wetu LAKINI pia pasipo kutumia faida yake yote katika kizazi hiki kupita kiasi bila kuangalia kizazi kingine kijacho. Kwa maana raslimali iliyopo licha ya kuoa faida kubwa kiuchumi kuna siku itakwisha! Je, sisi wa kizazi hiki ndio tuna haki pekee ya faida ya raslimali kama gesi toka Mtwara? HAPANA! Lazima tuungane na Rais JK pamoja na Mh. Ummy katika suala la "sustainable development" katika kila sekta ya uzalishaji nchini.



2 comments:

  1. Safi sana Mh Ummy kwa kuwajali watanzania. sustainable development ndio mpango mzima

    ReplyDelete
  2. Mipango endelevu ndio itiliwe mkazo hapa Tanzania ili kutunza mazingira na kulinda vizazi vijavyo

    ReplyDelete