Hongera Radio one stereo kwa kurusha matangazo kupitia internet. Hakika blogu hii imefurahishwa sana na Radio hii kwa kuwapasha habari mbalimbali watanzania walioko ndani na nje ya Tanzania. Kama mdau wa blogu hii ya tuijenge tanzania nimefurahi sana kupata habari za Tanzania kupitia Radio One kwa njia ya mtandao wa internet nikiwa nchini Sweden. Nikiwa Sweden nimeweza kusikiliza kipindi cha michezo cha saa moja na nusu usiku. Hakika nimeweza kumsikiliza live Maulid Kitenge kwenye kipindi hiki cha michezo. Pia unaweza kupata taarifa za moja kwa moja toka radio hii kwa vipindi vingine vingi kupitia internet. Hakika watanzania walioko nje ya Tanzania wanajifunia kuwa na radio hii.
Mtanzania yoyote aliye nje ya Tanzania anaweza kupata matangazo ya radio hii kupitia link hii. Hakika ukiwa popote pale duniani unapata uhondo na habari toka Tanzania kupitia radio hii. Aidha, ukiingia ndani ya ukurasa/link hii utakuta sura mbalimbali za watangazaji wa radio one kama vile Maulid Kitenge, Omary Katanga, Amina Chengo, Tumie Omary, Lugendo Madege, Isaac Gamba, Salma Dakota nk.
Blogu hii inaomba radio nyingine za Tanzania ziingie katika mfumo huu wa kimataifa ili kuwapasha watanzania habari mbalimbali.

Picha: ippmedia.com
Picha: ippmedia.com
No comments:
Post a Comment