Maktaba katika mashule ni suala ambalo Tanzania inatakiwa
kulitilia mkazo. Nchini Sweden, takriban shule zote kuanzia chekechea, msingi
mpaka sekondari kuna maktaba za shule. Maktaba hizi zinawasaidia wanafunzi
kupata vitabu, majalida na machapisho mbalimbali kwa ajili ya masomo yao. Vile
vile walimu nao hupata wasaa wa kutumia maktaba kwa ajili ya kuandaa mada mbali
mbali za masomo kwa ajili ya wanafunzi.
Tanzania tunatakiwa kuiga mfano huo wa kuwa na maktaba za
kisasa zenye vitabu, machapisho na majalida kwa ajili ya wanafunzi na walimu.
Hii itawasaidia sana wanafunzi kuongeza ujuzi na maarifa wa mambo wanayojifunza
shuleni.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inabidi itilie mkazo
suala la maktaba mashuleni kwa kuweka vitabu, majalida na machapisho kulingana
na mitaala husika na pia kuhakikisha wanaajili wakutubi waliohitimu toka
taasisi zinazotoa mafunzo ya kimaktaba. Hii itasaidia kuwezesha wanafunzi na
walimu kupata msaada wa kitaalamu toka kwa wataalamu (wakutubi).
Pia ni vyema kwa serikali kuwa na sera ya kuwa na maktaba
katika shule zetu na kuhakikisha wakaguzi wa shule wanakagua uwepo wa maktaba
za shule kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu.
Uwepo wa maktaba mashuleni unaongeza maarifa na ujuzi kwa
walimu na wanafunzi.

Picha: Mojawapo ya MAKTABA katika shule ya msingi nchini Sweden

Picha: Mojawapo ya MAKTABA katika shule ya msingi nchini Sweden
No comments:
Post a Comment