Thursday, April 27, 2017

Hongera kampuni ya simu ya ZANTEL kwa kuwa Mdhamini Mkuu "Main Sponsor" kwenye kongamano la kimataifa la jinsia" DUCE

Image may contain: sky and outdoor
Hongera kampuni ya simu ya ZANTEL kwa kuwa Mdhamini Mkuu "Main Sponsor" kwenye kongamano la kimataifa la jinsia" DUCE 1st International Conference on Gender in Higher Learning Institutions" lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).  Madhumuni ya kongamano hili la kimataifa ni kuibua mambo mbalimbali yahusuyo jinsia kwa mtizamo wa taasisi za elimu ya juu katika kutetea usawa wa kijinsia na haki za kibinadamu.

Tokeo la picha la zantel
Blogu hii inawapongeza sana na kwa hakika ZANTEL ni mfano wa kuigwa nchini. Aidha huduma za ZANTEL ni nzuri sana na hasa kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini. Blogu hii inatoa wito wa wanafunzi wa Elimu ya Juu na wananchi wengine kwa jumla kujiunga na ZANTEL.

Hongera Mh Ummy Mwalimu kwa kumwakilisha vyema Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwenye kongamano la kimataifa la jinsia

Hongera Mh Ummy Mwalimu kwa kumwakilisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwenye kongamano la kimataifa la jinsia" DUCE 1st International Conference on Gender in Higher Learning Institutions". Madhumuni ya kongamano hili la kimataifa ni kuibua mambo mbalimbali yahusuyo jinsia kwa mtizamo wa taasisi za elimu ya juu katika kutetea usawa wa kijinsia na haki za kibinadamu. 
Image may contain: 1 person, standing, car and outdoor
Blogu hii inatoa pongezi kwako hasa kwa hotuba nzuri sana. Hakika blogu hii imefuatilia hotuba uliyoitoa na kuzifanya taasisi za elimu ya juu (vyuo vikuu ikiwemo DUCE) kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo " ongezeko la wanafunzi wa kike na kiume kupitia elimu bure itolewayo na serikali mpaka kidato cha nne". Pia blogu hii imefurahishwa na kauli ya kuwahimiza wasichana na wanawake kuwa ELIMU ndio kila kitu sio sura au umbo zuri. 
Image may contain: 6 people, people standing and outdoor

Image may contain: 6 people, people standing, suit, wedding and outdoor
Aidha umesisitiza umuhimu na ulazima wa kutokatisha masomo watoto wa kike wanaopata mimba mashuleni. Hakika hili ni jambo jema na litaokoa wasichana wengi ambao wangekosa masomo kwa ajili ya mimba. 


Image may contain: 2 people, people standing

Image may contain: one or more people
Tatizo la mimba za watoto wa kike linaenda hasa kwa familia maskini nchini. Kitendo cha kutetea ELIMU kwa mtoto wa kike ni suala linalopaswa kuungwa mkono na kila mwananchi nchini Tanzania wakiwemo wabunge, madiwani, watunga sera, wataalamu wa elimu nk.
Image may contain: 3 people, people sitting

Image may contain: 6 people, crowd

Hongera sana Mh Ummy kwa kumwakilisha vyema Mama Samia Suluhu Hassan.


Image may contain: 3 people, people standing

Hongera uongozi wa DUCE kwa kuandaa kongamano la kimataifa la masuala ya jinsia nchini

Image may contain: tree, plant, sky, house, basketball court, outdoor and nature
Hongera Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE) kwa kuandaa kongamano la kimataifa la jinsia" DUCE 1st International Conference on Gender in Higher Learning Institutions". 
Image may contain: 2 people, people sitting
Kwa hakika madhumuni ya kongamano hili la kimataifa ni kuibua mambo mbalimbali yahusuyo jinsia kwa mtizamo wa taasisi za elimu ya juu katika kutetea usawa wa kijinsia na haki za kibinadamu. 
Image may contain: 3 people, people sitting
Blogu hii inatoa pongezi kwa uongozi mzima wa DUCE kwa kuandaa kongamano hili lililowakutanisha watafiti, wahadhiri na wanaharakati wa masuala ya jinsia na haki za kibinadamu duniani. Kwa maelezo zaidi tembelea hapa.
Image may contain: 6 people, people standing, suit, wedding and outdoor

Sunday, April 16, 2017

Hongera serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt Magufuli kwa uzinduzi ujenzi wa maghorofa ya Magomeni jijini Dar es Salaam

Tokeo la picha la magufuli MAGOMENI
Picha: ccm/ikulu
Hongera serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa uzinduzi ujenzi wa maghorofa ya Magomeni jijini Dar es Salaam. Siku ya jumamosi ya tarehe 15 Aprili 2017 Mh Rais aliweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa maghorofa mbalimbali kwa ajili ya wakazi wa Magomeni KOTA. Hakika manthari ya jiji la Dar es Salaam itabadilika mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huu mkubwa ambapo licha ya kuwahifadhi wakazi 644 waliokuwa wa Magomeni KOTA pia watu wengine watapata fursa ya kuishi katika majengo hayo. 


Blogu hii inampongeza Rais na inamwomba azidi kuwaletea watanzania maendeleo kupitia ujenzi wa makazi bora kwa gharama nafuu. Katika nchi zilizoendelea ujenzi wa namna hii ndio umeboresha makazi ya watu na kwa Tanzania ya Magufuli INAWEZEKANA.


Hongera Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutimiza AHADI na kuzindua Mabweni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Picha: tanzaniatoday

Hongera Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza ahadi yako ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Leo jumamosi 15 Aprili, 2017 Mh Rais amefungua rasmi mabweni yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi takribani 3,840.

Hakika blogu hii inampongeza sana Rais Mchapakazi kwa kutimiza ahadi na kuhakikisha ujenzi unaenda kwa kasi licha ya kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 10 tu. Katika hali tuliyozoea nyuma tungetegemea kiasi hiki kujenga mabweni chini ya nusu LAKINI chini ya uongozi wa HAPA KAZI TU malengo yametimia kwa kujenga mabweni yenye uwezo wa kuchukuwa wanafunzi wengi na kwa gharama nafuu na halisi. Blogu hii pia inaupongeza uongozi wa UDSM chini ya Mkuu wa Chuo Mh Dkt Jakaya Kikwete na Makamu wake Prof Rwekaza Mkandala kwa kufanikisha ukamilifu wa mabweni haya na hasa kwa UDSM kugharamia ununuzi wa vitanda, meza, viti na magodoro.  

Aidha blogu hii inaupongeza uongozi wa Wakala wa Majengo (TBA) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kujenga mabweni 20 yenye ghorofa nne pamoja na uzio. 

Blogu hii inaomba serikali kuendelea kujenga mabweni na hasa mabweni ya WASICHANA katika vyuo vingine vya umma na hasa Chuo Kishiriki cha Elimu (DUCE) ambapo wanafunzi wengi wanapanga nje ya chuo na wakati wa usiku inakuwa si salama kwa wanafunzi.

Kwa uzoefu uliopo blogu hii ingependa mabweni haya wapewe wanafunzi wa jinsi yote na hasa wa kike, na wale wenye changamoto mbalimbali.

Blogu hii inaomba UDSM kutilia maanani utunzaji na ukarabati wa mabweni haya mara kwa mara. 

Wednesday, April 12, 2017

Hongera serikali ya Tanzania kwa uzinduzi ujenzi wa reli ya kisasa

Tokeo la picha la rapind train
Picha: youtube
Hongera serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa uzinduzi ujenzi wa reli ya kisasa "standard gauge" ambayo itatoka Pugu mjini Dar es Salaam mpaka Morogoro kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa. Uzinduzi umefanyika leo jumatano tarehe 12 Aprili 2017 katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam na mradi huo unatarajiwa kutumia kiasi cha Trilioni 2.7 fedha za kitanzania. Hizi ni pesa toka kwa serikali ya Tanzania pekee na ni mfano mzuri kwa maendeleo ya taifa.

Kinachofurahisha ni kuwa reli hii itatumia umeme katika uendeshaji wake na kufanya iwe na kasi kubwa katika kusafirisha abiria na mizigo. Kiukweli, kama reli hii itakamilika, Tanzania itakuwa mfano bora barani Afrika kama nchi za South Africa na Morroco zenye aina hii ya reli. Nchi zilizoendelea duniani ndizo zinatumia reli za namna hii na hasa zinazoendeshwa na umeme.

Reli hiyo licha ya kusaidia abiria kusafiri kwa muda mfupi pia ina uwezo mkubwa wa kubeba mizigo mingi kwa wakati mmoja tofauti na reli za zamani. Hii itachochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania na nchi jirani. Ni matarajio ya blogu hii kuwa ujenzi wa reli ya kisasa utaendelea mpaka kwenye mikoa ya Kigoma na Mwanza na kuunganisha Tanzania na nchi jirani. Hii itasaidia pia kuokoa uharibifu wa barabara zetu zilizojengwa kwa gharama kubwa ambapo zinatumika sasa kusafirisha magari makubwa yakiwemo malori ya mizigo.

Blogu hii inaomba serikali kuingia mikataba ya kujenga reli hii ya kisasa kwa vipande vipande ili kuharakisha ukamilifu wa reli hii mpaka mikoa ya Mwanza na Kigoma. Pia serikali isisahu mikoa mingine kama vile ya kusini, nyanda za juu na kaskazini katika kujenge reli za namna hii.

Hakika hili jambo linastahili kupongezwa na kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo wa nchi yetu.

Wednesday, April 5, 2017

Picha BORA kwa mujibu wa TUIJENGE TANZANIA

Picha: twitter.com (Jakaya Kikwete)

Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mama Mh Salma Rashid Kikwete pamoja na kijana wao nadhifu nje ya ukumbi wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dodoma. Mama Salma amekula kiapo cha kuwa MBUNGE ktk Bunge la Muungano, 04/04/2017

Kila la kheri Serengeti boys katika michuano ya AFRICA nchini GABON

Tokeo la picha la serengeti boys
Picha: goal.com

Kila la kheri Serengeti boys (Timu ya Taifa chini ya miaka 17). Jana 04/04/2017 timu yetu ilikabidhiwa bendera na Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, mama Samia SULUHU kwa ajili ya ushiriki wa michuano ya AFRICA itakayofanyika mapema GABON. Kila mtanzania ana imani na timu hii hasa kutokana na maandalizi yaliyokwishafanyika na pia morali na ustadi wa wachezaji, benchi la ufundi, kamati mbalimbali, na TFF. Blogu hii kwa hali ya kipekee inampongeza Rais wa TFF Jamal MALINZI kwa kuiandaa vyema timu hii. Kwa hili MALINZI anastahili pongezi. Aidha blogu hii inawapongeza wadau wengine waliosaidia na wanaoendelea kusaidia timu hii kwa namna moja na nyingine. 

Hongera Profesa MKUMBO kwa kuteuliwa na Rais kuwa Katibu Mkuu (Wizara ya Maji na Umwagiliaji)

Tokeo la picha la kitila mkumbo
Picha: twitter.com

Hongera Profesa Kitila MKUMBO kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Katibu Mkuu (Wizara ya Maji na Umwagiliaji). Blogu hii kwanza inampongeza Rais Dkt John Pombe MAGUFULI kwa kufanya maamuzi adimu ya kumteua Profesa MKUMBO. Uteuzi huu uwe changamoto kwa MKUMBO katika kufanya kazi kwa ustadi, weledi, uadilifu na kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi. Uteuzi huu utazidi kukumbukwa katika historia ya Tanzania kwa sababu bado nchi yetu ni changa, hasa katika siasa za vyama vingi. Profesa MKUMBO kabla ya uteuzi huu alikuwa mhadhiri wa saikolojia katika Shule ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia mshauri wa chama cha upinzani ACT Wazalendo.

Blogu hii inamtakia kila la kheri Profesa MKUMBO katika utendaji wake mpya wa kazi. Hakika hapa ni kazi TU.