
Hongera Mh Ummy Mwalimu kwa kumwakilisha Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwenye kongamano la kimataifa la jinsia" DUCE 1st International Conference on Gender in Higher Learning Institutions". Madhumuni ya kongamano hili la kimataifa ni kuibua mambo mbalimbali yahusuyo jinsia kwa mtizamo wa taasisi za elimu ya juu katika kutetea usawa wa kijinsia na haki za kibinadamu.

Blogu hii inatoa pongezi kwako hasa kwa hotuba nzuri sana. Hakika blogu hii imefuatilia hotuba uliyoitoa na kuzifanya taasisi za elimu ya juu (vyuo vikuu ikiwemo DUCE) kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo " ongezeko la wanafunzi wa kike na kiume kupitia elimu bure itolewayo na serikali mpaka kidato cha nne". Pia blogu hii imefurahishwa na kauli ya kuwahimiza wasichana na wanawake kuwa ELIMU ndio kila kitu sio sura au umbo zuri.
Aidha umesisitiza umuhimu na ulazima wa kutokatisha masomo watoto wa kike wanaopata mimba mashuleni. Hakika hili ni jambo jema na litaokoa wasichana wengi ambao wangekosa masomo kwa ajili ya mimba.

Tatizo la mimba za watoto wa kike linaenda hasa kwa familia maskini nchini. Kitendo cha kutetea ELIMU kwa mtoto wa kike ni suala linalopaswa kuungwa mkono na kila mwananchi nchini Tanzania wakiwemo wabunge, madiwani, watunga sera, wataalamu wa elimu nk.






Hongera sana Mh Ummy kwa kumwakilisha vyema Mama Samia Suluhu Hassan.

No comments:
Post a Comment