Wednesday, April 5, 2017

Kila la kheri Serengeti boys katika michuano ya AFRICA nchini GABON

Tokeo la picha la serengeti boys
Picha: goal.com

Kila la kheri Serengeti boys (Timu ya Taifa chini ya miaka 17). Jana 04/04/2017 timu yetu ilikabidhiwa bendera na Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, mama Samia SULUHU kwa ajili ya ushiriki wa michuano ya AFRICA itakayofanyika mapema GABON. Kila mtanzania ana imani na timu hii hasa kutokana na maandalizi yaliyokwishafanyika na pia morali na ustadi wa wachezaji, benchi la ufundi, kamati mbalimbali, na TFF. Blogu hii kwa hali ya kipekee inampongeza Rais wa TFF Jamal MALINZI kwa kuiandaa vyema timu hii. Kwa hili MALINZI anastahili pongezi. Aidha blogu hii inawapongeza wadau wengine waliosaidia na wanaoendelea kusaidia timu hii kwa namna moja na nyingine. 

No comments:

Post a Comment