Picha: youtube
Hongera serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa uzinduzi ujenzi wa reli ya kisasa "standard gauge" ambayo itatoka Pugu mjini Dar es Salaam mpaka Morogoro kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa. Uzinduzi umefanyika leo jumatano tarehe 12 Aprili 2017 katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam na mradi huo unatarajiwa kutumia kiasi cha Trilioni 2.7 fedha za kitanzania. Hizi ni pesa toka kwa serikali ya Tanzania pekee na ni mfano mzuri kwa maendeleo ya taifa.
Kinachofurahisha ni kuwa reli hii itatumia umeme katika uendeshaji wake na kufanya iwe na kasi kubwa katika kusafirisha abiria na mizigo. Kiukweli, kama reli hii itakamilika, Tanzania itakuwa mfano bora barani Afrika kama nchi za South Africa na Morroco zenye aina hii ya reli. Nchi zilizoendelea duniani ndizo zinatumia reli za namna hii na hasa zinazoendeshwa na umeme.

Reli hiyo licha ya kusaidia abiria kusafiri kwa muda mfupi pia ina uwezo mkubwa wa kubeba mizigo mingi kwa wakati mmoja tofauti na reli za zamani. Hii itachochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania na nchi jirani. Ni matarajio ya blogu hii kuwa ujenzi wa reli ya kisasa utaendelea mpaka kwenye mikoa ya Kigoma na Mwanza na kuunganisha Tanzania na nchi jirani. Hii itasaidia pia kuokoa uharibifu wa barabara zetu zilizojengwa kwa gharama kubwa ambapo zinatumika sasa kusafirisha magari makubwa yakiwemo malori ya mizigo.
Blogu hii inaomba serikali kuingia mikataba ya kujenga reli hii ya kisasa kwa vipande vipande ili kuharakisha ukamilifu wa reli hii mpaka mikoa ya Mwanza na Kigoma. Pia serikali isisahu mikoa mingine kama vile ya kusini, nyanda za juu na kaskazini katika kujenge reli za namna hii.
Hakika hili jambo linastahili kupongezwa na kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo wa nchi yetu.
No comments:
Post a Comment