
Picha: tanzaniatoday
Hongera Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza ahadi yako ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Leo jumamosi 15 Aprili, 2017 Mh Rais amefungua rasmi mabweni yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi takribani 3,840.
Hakika blogu hii inampongeza sana Rais Mchapakazi kwa kutimiza ahadi na kuhakikisha ujenzi unaenda kwa kasi licha ya kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 10 tu. Katika hali tuliyozoea nyuma tungetegemea kiasi hiki kujenga mabweni chini ya nusu LAKINI chini ya uongozi wa HAPA KAZI TU malengo yametimia kwa kujenga mabweni yenye uwezo wa kuchukuwa wanafunzi wengi na kwa gharama nafuu na halisi. Blogu hii pia inaupongeza uongozi wa UDSM chini ya Mkuu wa Chuo Mh Dkt Jakaya Kikwete na Makamu wake Prof Rwekaza Mkandala kwa kufanikisha ukamilifu wa mabweni haya na hasa kwa UDSM kugharamia ununuzi wa vitanda, meza, viti na magodoro.
Aidha blogu hii inaupongeza uongozi wa Wakala wa Majengo (TBA) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kujenga mabweni 20 yenye ghorofa nne pamoja na uzio.
Blogu hii inaomba serikali kuendelea kujenga mabweni na hasa mabweni ya WASICHANA katika vyuo vingine vya umma na hasa Chuo Kishiriki cha Elimu (DUCE) ambapo wanafunzi wengi wanapanga nje ya chuo na wakati wa usiku inakuwa si salama kwa wanafunzi.
Kwa uzoefu uliopo blogu hii ingependa mabweni haya wapewe wanafunzi wa jinsi yote na hasa wa kike, na wale wenye changamoto mbalimbali.
Blogu hii inaomba UDSM kutilia maanani utunzaji na ukarabati wa mabweni haya mara kwa mara.
Blogu hii inaomba UDSM kutilia maanani utunzaji na ukarabati wa mabweni haya mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment