
Picha: ccm/ikulu
Hongera serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya
Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa uzinduzi ujenzi wa maghorofa ya Magomeni
jijini Dar es Salaam. Siku ya jumamosi ya tarehe 15 Aprili 2017 Mh Rais aliweka
jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa maghorofa mbalimbali kwa ajili ya wakazi
wa Magomeni KOTA. Hakika manthari ya jiji la Dar es Salaam itabadilika mara
baada ya kukamilika kwa ujenzi huu mkubwa ambapo licha ya kuwahifadhi wakazi 644 waliokuwa wa Magomeni KOTA pia watu wengine watapata fursa ya kuishi katika
majengo hayo.
Blogu hii inampongeza Rais na inamwomba azidi kuwaletea
watanzania maendeleo kupitia ujenzi wa makazi bora kwa gharama nafuu. Katika
nchi zilizoendelea ujenzi wa namna hii ndio umeboresha makazi ya watu na kwa
Tanzania ya Magufuli INAWEZEKANA.
No comments:
Post a Comment