Wednesday, April 5, 2017

Hongera Profesa MKUMBO kwa kuteuliwa na Rais kuwa Katibu Mkuu (Wizara ya Maji na Umwagiliaji)

Tokeo la picha la kitila mkumbo
Picha: twitter.com

Hongera Profesa Kitila MKUMBO kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Katibu Mkuu (Wizara ya Maji na Umwagiliaji). Blogu hii kwanza inampongeza Rais Dkt John Pombe MAGUFULI kwa kufanya maamuzi adimu ya kumteua Profesa MKUMBO. Uteuzi huu uwe changamoto kwa MKUMBO katika kufanya kazi kwa ustadi, weledi, uadilifu na kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi. Uteuzi huu utazidi kukumbukwa katika historia ya Tanzania kwa sababu bado nchi yetu ni changa, hasa katika siasa za vyama vingi. Profesa MKUMBO kabla ya uteuzi huu alikuwa mhadhiri wa saikolojia katika Shule ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia mshauri wa chama cha upinzani ACT Wazalendo.

Blogu hii inamtakia kila la kheri Profesa MKUMBO katika utendaji wake mpya wa kazi. Hakika hapa ni kazi TU. 

No comments:

Post a Comment