Tuesday, August 20, 2013

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) likiongozwa na Ndg Nehemiah Mchechu linastahili pongezi za dhati kabisa

Hakika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) hivi sasa linapiga hatua kubwa katika ujenzi wa majengo madogo na makubwa, ya makazi na ya kibiashara. Kasi yao inayoonekana hapa jijini Dar es Salaam. Blogu hii imejaribu kutembelea baadhi ya miradi inayoondeshwa na NHC na kujionea ubora wa hali ya juu katika ujenzi wa majengo. Mifano ipo mingi sana. Tunasema ubora tuna maana viwango na ukamilifu wa jengo na mazingira yake. Kwa kawaida tumezoea kuona majengo yakijengwa bila ya kujali sehemu ya nje ya jengo ikoje. Lakini NHC kwenye majengo yao wanayojenga wanazingatia ukamilifu kama vile kuweka uzio, kuweka vitofali kuzuia vumbi na michanga pamoja na kufanya sehemu kutokuwa na tope wakati wa mvua. Viwango hivyi ni vya kimataifa.

Hivi sasa NHC itajenga majengo haya yanayoonekana kwenye picha hii. Hakika NHC pamoja na uongozi wake ukiongozwa na mkurugenzi wake mkuu Ndg Nehemiah Mchechu kwa ujumla unastahili pongezi za dhati kabisa. Blogu hii inaomba NHC wazidi kujenga majengo kwa wingi hapa nchini na hasa pia kwa wananchi wa kipato cha chini na kati ambao wapo wengi.

Picha: National Housing Corporation facebook page


Pongezi kwa klabu ya Simba kwa kuruhusu SHOMARI KAPOMBE kucheza ufaransa kwa makubaliano maalum

Pongezi kwa Simba Football Club kwa kuruhusu mchezaji hodari na chipukizi Shomari Kapombe kuchezea timu ya daraja la nne AS Cannes iliyoko nchini ufaransa kwa makubaliano maalum. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba Mh. Ismail Aden Rage, klabu ya Simba imekubali Kapombe achezee timu hiyo kwa makubaliano ya kumtafutia timu nyingine ya kucheza ndani ya kipindi cha miaka miwili kuanzia sasa. Klabu hii ya AS Cannes ndio iliyowakuza wachezaji kama Patrick Vieira, Zinedine Zidane na Luis Hernandez.
Blogu hii kwa dhati kabisa imefurahishwa na klabu ya SIMBA kwa kuwawezesha wachezaji hasa chipukizi kupata timu za nje ya Tanzania. Mfano wa SIMBA kupeleka na kuuza wachezaji nje ni kwa Mbwana Samata aliyekwenda TP MAZEMBE, DRC, Emmanuel Okwi aliyekwenda Tunisia na wengine wengi. Hakika mafanikio ya wachezaji hawa siyo yao binafsi tu bali ni kwa taifa zima. 
Blogu hii inaamini KAPOMBE ni mchezaji mzuri ambaye siku moja atakuwa sawa na wachezaji wengine maarufu kama Didier Drogba, Samuel Etoo, Emmanuel Adebayor, Fredrick Kanoute, Kolo Toure, Yaya Toure, Michael Essien, John Mikel Obi na wengineo wengi. Pia fedha na utajiri atakaopa Kapombe kwa hakika utaisaidia Tanzania kwa namna moja ama nyingine, mbali na kuitangaza nchi kwenye ramani ya dunia.
 Blogu hii inapenda kuziomba klabu nyingine hapa Tanzania kuiga utamaduni huu wa SIMBA SPORTS CLUB.
Shomari Kapombe 
Picha:  http://www.24tanzania.com

Pongezi za dhati kwa Dr Stergomena Tax kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa SADC kwa kipindi cha 2013 - 2017

Mwanzo wa kunukuu "Ni furaha kubwa kwangu kwa Dr. Stergomena Tax (Mwanamke toka Tanzania) kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa SADC kwa kipindi cha 2013 -2017. Hii ni mojawapo ya vielelezo vingi kuwa WANAWAKE WANAWEZA! Hongera sana Dr. Tax, Hongera sana Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe Benard Membe kwa kazi nzuri. Hongera nyingi zaidi kwa Mhe. Rais, Jakaya Kikwete kwa kuwekeza na kuamini kwa dhati katika Uongozi wa Wanawake (Women Leadership). Sifa nzuri ya Tanzania inazidi kupaa! Kila la kheri Dr. Tax ktk Utekelezaji wa Majukumu yako Mapya." Mwisho wa kunukuu (Mh Ummy Mwalimu - Mbunge, Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto)
Blogu hii inapenda kutoa pongezi za dhati kwa Dr Stergomena Tax kwa kuaminiwa na kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa SADC. Pia blogu hii inapenda kuwashukuru waliochangia mafanikio ya mama huyu hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete. Pia blogu hii inapenda kumshukuru Mh Ummy Mwalimu kwa taarifa hii njema kwa watanzania. HAKIKA WANAWAKE WANAWEZA, TUZIDI KUWAAMINI!
Picha:http://www.wavuti.comPicture

Monday, August 19, 2013

Pongezi kwa bilionea Dangote kwa ujenzi wa kiwanda cha saruji mtwara nchini Tanzania

Blogu hii inapenda kutoa pongezi za dhati kwa kiwanda cha Dangote kinachotarajiwa kujengwa na kuanza uzalishaji wa saruji nchini kupitia mkoa wa mtwara. Kiwanda hiki kinatarajiwa kuzalisha takribani tani milioni 3 za saruji kwa mwaka ikiwa ni mifuko 150,000 kwa siku. Hakika kiwango hicho ni kikubwa na pia kwa kufanya hivyo kiwanda hicho kitatoa ajira za kudumu zipatazo elfu moja na zisizo za kudumu zipatazo elfu tisa. Kiwanda hiki ambacho mmiliki wake ni bilionea Dangote amewekeza takribani dola 500 USA $ (trilioni 8 za kitanzania) kwa ajili ya ujenzi huo. Ujenzi wa kiwanda hiki ulizinduliwa Waziri Mkuu Mizengo Mh. Pinda kwa kuweka jiwe la msingi. (chanzo: mwananchi).Kwa habari zaidi wasiliana na mwananchi.

Blogu hii inapenda kuwahamasisha wawekezaji wengine wa ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye uzalishaji wa saruji kwa kuwa mahitaji bado ni makubwa sana.







Picha na coastalforests.tfcg.org

Wednesday, August 14, 2013

Maneno ya busara toka kwa Mh. Husna Mbwambo ambayo ni "Empowering the powerless is Development"

Blogu hii inapenda kutoa maneno ya busara toka kwa Mh. Husna Mbwambo: 
Mwanzo wa kunukuu "Empowering the powerless is Development" mwisho wa kunukuu. 
Blogu hii inatoa tafsiri isiyo rasmi ya maneno kwenda kwenye kiswahili "Kuwezesha wasionacho ni Maendeleo". Hakika maneno haya ni mazuri ambayo yanastahili kuigwa na wengine ili kuleta ustawi katika maisha ya mwanadamu. Blogu hii inampongeza Mh. Husna kwa busara zake.  Asante!!

Hongera TRA kwa kuanzisha mfumo wa kieletroniki wa kulipia ada za magari kupitia mtandao kama vile TIGOPESA, M-PESA, AIRTEL MONEY, MAXMALIPO na Benki

 
Hongera Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuanzisha mfumo wa kieletroniki wa kulipia ada za magari kwa njia ya mtandao. Huduma hii imeanza mwezi 08 mwaka 2013 kupitia simu za viganjani (M-PESA, AIRTELMONEY, TIGOPESA), benki na watoa huduma wengine wa kimtandao. Juhudi hizi za TRA mbali na kuwarahisishia wateja na adha ya foleni walizokuwa wakizipata awali pamoja na kupoteza muda pia inatoa fursa kwa taifa kuwa na huduma bora kwa walipakodi na kufanya mapato ya Serikali kukusanywa kikamilifu. Mapato haya ndiyo yanayowezesha serikali kutoa huduma bora kwa jamii ya kitanzania pamoja na kuleta maendeleo. 

Blogu hii inapenda kuwaelimisha wananchi namna huduma hii mpya inavyofanya kazi:
  1. Kufahamu kiwango cha kodi. Tuma ujumbe wenye neno “Kadiria” au “Assess” acha nafasi andika namba za  gari mfano KADIRIA T171AUC kwenda namba 15341.  
  2. Kulipa: Tuma ujumbe wenye neno; “sajili” acha nafasi na kuandika namba ya gari husika. Tuma ujumbe huo kwenda namba15341. Baada ya hapo mlipakodi atapata ujumbe wa namba ya kumbukumbu ya malipo (Reference number).
  3. Fanya malipo kwa kutumia TIGOPESA, AIRTELMONEY, MPESA au MAXMALIPO kwa kutumia namba ya kumbukumbu uliyopata.
  4. Kuchukua cheti: (sticker ya gari): nenda katika ofisi yoyote ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ukiwa na namba ya kumbukumbu uliyofanyia malipo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Blogu hii inapenda kutoa pongezi za dhati kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa juhudi hii. Pia blogu hii inaomba taasisi zingine ziige ili kumkomboa mtanzania na kuleta maendeleo kwa kasi. Hakika pamoja tunajenga TAIFA

Monday, August 12, 2013

Hongera Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Mh. Vrajilal Jituson kwa kutoa msaada wa kompyuta jimboni

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini mkoani Manyara, Mh. Vrajilal Jituson ametoa kompyuta mbili (Laptop) kwa ajili ya waandishi wa habari wa mkoa huo. Msaada huo kusudi lake ni kuwawezesha waandishi waweze kuandika habari za vijijini. Mbunge huyo ambaye pia ni mwanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa huo kupitia Mfuko wa Ofisi yake ameazimia kutoa kompyuta zipatazo ishirini na nane kwenye maeneo tofauti tofauti jimboni kwake ili kurahisisha utendaji kazi wa taasisi mbalimbali.
Chanzo: Mwananchi

Blogu hii inapenda kumpongeza kwa dhati Mh. Vrajilal Jituson kwa kujitolea na kuwasaidia wengine katika ujenzi wa taifa letu. Pia, blogu hii inaomba utamaduni huu uendelezwe na wengine waige.

Picha: mireranitanzanite.blogspot.com

Tuesday, August 6, 2013

Umuhimu wa vijana wasomi katika kulinda na  kumiliki rasilimali za taifa, sera na katiba ni jambo jema

Mkutano uliofanyika tarehe 5 Agosti 2013 mijini DSM  kuhusu umuhimu wa vijana wasomi katika kulinda na kumiliki rasilimali za taifa, sera na katiba ni jambo jema linalotakiwa kuenziwa. Katika mkutano huo  Prof Muhongo akiwa kama waziri wa nishati na mtaalamu wa giolojia na madini alizungumzia rasilimali za taifa, nishati, gesi na umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu. Wakati Dr. Frateline Mlashani Kashaga alizungumzia sera, rasilimali na vijana akiwa kama mtaalamu wa sera (policy analyst). Wakili Mmanda aliongelea rasimu ya katiba na rasilimali za taifa. Hakika vijana hawatakiwi kusahauliwa katika kulinda na kumiliki rasilimali za taifa. Blogu hii inapongeza juhudi hizi na inaomba ziwe endelevu.
Photo: Minister of Energy and Minerals of Tanzania, Professor Muhongo presenting his paper on management of natural resouces and the role of youth, university students and graduates.
Picha: Dr. Frateline Mlashani Kashaga

Monday, August 5, 2013

Hongera Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutokomeza malaria toka asilimia 25 mpaka chini ya 1

Hongera serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kupambana na kutokomeza malaria. Hakika juhudi hizi ni za kupongezwa maana ZANZIBAR imeweza kupambana na malaria kutoka kiwango cha asilimia 25 mpaka kufikia asilimia chini ya 1. Hata rais mstaafu wa Marekali Bill Clinton ameona na kutambua juhudi hizo na kuahidi kuzidi kuisaidia ZANZIBAR. Ugonjwa wa malaria ndio chanzo kikuu cha vifo kusini mwa jangwa la sahara na wanaoathilika zaidi ni watoto walio chini ya miaka mitano. Juhudi hizi zifanywe pia na upande wa pili wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ili kuokoa vifo vinavyoweza kuzuilika.

Picha: sundayshomari.com

Saturday, August 3, 2013

Hongera kwa mwekezaji aliyejenga KIBO COMPLEX Tegeta jijini DSM

Hongera kwa mwekezaji aliyejenga KIBO Complex iliyopo Tegeta Kibaoni.Ndani ya Kibo complex kuna huduma nyingi kama vile mabenki (NMB na CRDB), ATM mbalimbali, super market, maduka ya nguo, simu na vifaa vya kieletroniki, bar na sehemu za chakula na vinywaji laini, ukumbi bomba wa disco.Kuna parking na ulinzi wa kutosha. Hakika wakazi wa tegeta wanafarijika sana. Tunaomba wawekezaji wengine wawekeze kwenye maeneo yaliyo nje ya miji ili wananchi wengi waweze kupata huduma hii. Ujenzi wa miundo mbinu kama hii mbali na kuinua uchumi kwa maeneo yaliyo nje ya mji pia unapunguza foleni na msongamano katikati ya miji na majiji. Kazi kwenu halmashauri za mji na majiji kuhamasisha uwekezaji wa namna hii.

Thursday, August 1, 2013

Hongera TCRA kwa kuzindua kampeni ya kuelimisha wananchi juu ya matumizi mazuri ya mawasiliano

Hongera TCRA kwa kuzindua kampeni nzuri ya kuelimisha jamii ya kitanzania juu ya matumizi mazuri ya mawasiliano. Katika uzinduzi huo TCRA imewatahadharisha wananchi kwa ujumla kutotumia fursa ya kukua kwa kasi kwa teknolojia ya mawasiliano vibaya, kama ilivyoanishwa katika Sheria ya Kielectroniki na Posta ya mwaka 2010. Blogu hii inapenda kuipongeza TCRA na mkurugenzi wake mkuu kwa kampeni hii. Pia blogu hii inapenda kampeni hii iwe endelevu.
Picha na chanzo cha habari: ippmedia.com