Hakika Azam TV na TBC1 mnastahili pongezi za dhati. Azam TV kwa sasa inaonyesha michezo ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Azam TV wameonyesha mapinduzi makubwa katika soka nchini kwa kuonyesha michezo ya ligi kuu kwa kiwango bora na cha kimataifa. Nchi jirani zinaonyesha ligi zao kupitia vituo vingine vya nchi za ng'ambo. Hakika watanzania na hasa wana wanamichezo wanajivunia mafanikio haya ya Azam TV.
Juhudi hizi za Azam TV zinastahili kuungwa mkono na wadau wote wa michezo ikiwemo serikali. Thamani ya mpira wa Tanzania itakuwa kwa msaada wa Azam TV. Vile vile wachezaji kitanzania wataonekana kimataifa na kufanya soko lao kuwa kubwa.
Picha:deejaydeo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment