Hongera serikali ya Tanzania kwa kuanzisha Tume
ya TEHAMA “ICT” nchini Tanzania. Hakika hatua hii ya serikali ni ya kuungwa
mkono. Wadau wa TEHAMA nchini tumefurahi na kufarijika sana baada ya kusikia
serikali ipo kwenye mchakato wa kuanzisha tume ya TEHAMA. Tume hii itaratibu,
itasimamia na kuendeleza shughuli zote ya TEHAMA nchini. Sekta hii ya TEHAMA
inakuwa kwa kasi sana duniani na hapa nchini. Sekta hii pia inaingia kwenye
kila nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Hivyo ili Tanzania iwe na
mafanikio kupitia sekta hii, Tume ya kuratibu TEHAMA ni ya umuhimu sana.
Kwa uchache, TEHAMA ina chagamoto zake kama vile uwepo suala
la usalama wa taarifa za watu mbalimbali (e-security), haki ya faragha
(e-privacy), pamoja na haki ya wanachi
kupata taarifa (freedom of information). Mambo haya kwa kweli yana umuhimu wake
lakini yanakinzana. Nchi mbalimbali bado zinachangamoto ya kuweka mstari kati
ya haya mambo matatu.
Hivyo basi pamoja na mambo mengine Tume hii tunatarajia
itakuja na mfumo ama uwezo wa kulinganisha masuala haya matatu ili yasilete
athari nchini.
Pia ni wakati muafaka kwa serikali kupitia tume hii
kuanzisha sera mbalimbali za TEHAMA kama vile sera ya mitandao ya kijamii
(social media policy), sera ya mkonga wa internet (broadband internet policy)
pamoja na kupitia tena sera ya TEHAMA ya mwaka 2003 (ICT policy of 2003). Sera
hii imekaa kwa muda mrefu na inahitaji mapitio “review”.
Kuna mambo mengi sana ambayo tume hii ina kazi kubwa ya
kufanya. Lingine ni kuhamasisha na kutoa kipaumbele sehemu za vijijini kuwa na
TEHAMA na huduma za internet na data. Njia mojawapo ni kwa tume kuweka “incentive”
kwa makampuni ama watu wataowekeza vijijiji ili taifa letu liweze kupiga kasi
inayostahili. Incentive hii inaweza kuwa kwenye kodi.
Hakika kuna mambo mengi ya kufanya, hivyo kama wadau
tunaipongeza sana serikali kwa kuwa na wazo hili la kuanzisha tume ya TEHAMA
nchini. Hakika tupo pamoja na tutaendelea kushirikiana kuhakikisha TEHAMA
inakuza uchumi na kuleta ustawi nchini.
Picha: sundayshomari.com

Afisa Habari Mwandamizi toka Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Bi. Prisca Ulomi(kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu Uanzishwaji wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO)
No comments:
Post a Comment