Hongera
serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kujenga
kituo maalum katika chuo kikuu kishiriki cha DUCE kiitwacho "Teachers
Professional Center". Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Gharib Bilal alikuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo ya
uzinduzi iliyofanyika Jumatano ya tarehe 23 mwezi wa kumi mwaka 2013.
Aidha
kama mdau nilipata fursa ya kutoa mada mbele ya Makamu wa Rais Mh Gharib Bilal
jinsi gani kituo cha "Teacher Professional Center" kinachomilikiwa na
DUCE kinavyoweza kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika
kuchangia ubora wa Elimu nchini na hasa kuweza kuwapa maarifa na ujuzi walimu
(in-service teachers) kupitia Teknolojia ya kisasa ili kuongeza maarifa kwa
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini na kuongeza ufaulu.
Uzinduzi
wa kituo hiki unaenda pamoja na kauli mbiu ya "Big Results Now" yaani
"Matokeo Makubwa Sasa" katika sekta ya elimu nchini Tanzania.
Blogu
hii inapenda kuipongeza serikali ya Tanzania chini ya Mh Rais Jakaya Kikwete
kwa ujenzi wa kituo hiki maalum kitakacho chochea kasi ya elimu nchini na hasa
kitakachokuwa kikitumika kutoa mafunzo kwa walimu walio makazini kupitia
Teknolojia ya kisasa. Aidha blogu hii inakipongeza chuo kikuu kishiriki cha Elimu
DUCE kwa kuweza kutekeleza ujenzi wa kituo hiki. Vile vile blogu hii
inawapongeza wadau na wafanyakazi wa DUCE pamoja na Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi katika kusimamia ujenzi wa kituo hiki.
Pia
blogu hii inatoa pongezi na shukrani za pekee kwa Benki ya Dunia (World Bank)
kupitia mpango mahsusi uitwao "Science Technology and Higher
Education Program (STHEP) " uliofanikisha miradi mingi nchini kwenye
sekta ya elimu juu ukiwemo mradi huu wa wa ujenzi wa "Teacher
Professional Center" ndani ya chuo kikuu kishiriki cha DUCE.
Blogu
hii inaomba kituo hiki kitunzwe na pia kitumike kikamilifu ili kukizi lengo la
kituo chenyewe pamoja na kufikia malengo ya BIG RESULTS NOW! Pamoja tutafika!


















No comments:
Post a Comment