Nilichoongea wakati wa uzinduzi wa jengo la " Teachers Professional Center" pale DUCE, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu! hakikuwa kitu cha ajabu sana. Ni mambo wenzetu wanayoyafanya siku zote. Kwa dunia ya sasa huwezi kwenda kasi ya maendeleo bila ya kukopa toka ICT. Huwezi kuwafikia walimu ambao ndio nguzo ya taifa bila ICT. Nitawapa mfano mmoja ili mwanafunzi wa kawaida aelewe somo vizuri bila kukalili lazima ASOME (hapa sisi walimu wengi ndio tunapoteza nguvu zetu! Kuwasomea wanafunzi tukizani tunawafundisha! Hiyo haitoshi!), AONE (hapa ndipo wenzetu wanapotuacha na ndio wanatilia mkazo -ICT inaingia hapa unaweza tumia ICT kutengeneza animations ukaziweka kwenye CD au ukachukua video kuelezea concept ya "reproduction" badala ya kulazimisha kuwasomea), na KUTENDA (hapa pia wenzetu nchi zingine wanatupiga bao! Hatufanyi hivyo kwa visingizio kibao eti hakuna mahabara nk wakati waweza tumia ICT ama vitu vinavyopatikana kwenye mazingira yako na wanafunzi wakafanya na kuelewa somo! Mfano tuna vyura wengi kwenye mazingira yetu na kwenye baadhi ya mitihani ya kidato cha nne wanafunzi wanatakiwa kufanya practicals za kupasua vyura lakini ni mara ngapi walimu wa biology wanafanya practical hizo kwa wanafunzi wao ili kuwaelewa concepts kwa vitendo? Ila tunasingizia hatuna vifaa wakati tuna mapanya tena mapanya buku mitaani bila kuacha machura yanayotupigia kelele usiku). Kwa kifupi nilichozungumza sio kitu kigeni ila ni utamaduni wetu wa kutotumia fursa kama walimu na wadau wa elimu. Teknolojia niliyozungumza ambayo yaweza saidia "in-service teachers" vyuo vingi wanatumia kule University of UP Daudi Danda unajua mambo online teaching ya illuminate! Sasa kwa jinsi gani teknolojia hiyo inaweza kutusaidia kuwapa maarifa na ujuzi walimu wetu kwa gharama nafuu! Maana sio rahisi kuleta walimu wote kwenye chuo kama DUCE na kuwapa mbinu za kisasa bila ya kutumia teknolojia!
Mdau: Geofrey Kalumuna
No comments:
Post a Comment