Hongera eGA (serikali matandao) kwa kuwa na mpango mkakati wa miaka mitano, kuanzia mwaka 2012/13 mpaka 2016/17. Shabaha kubwa katika mpango huo mkakati ni kuziwezesha idara zote na taasisi za serikali zikiwemo wizara zote nchini pamoja na serikali za mitaa kutumia TEHAMA katika shughuli za kila siku za utendaji ili kuongeza uwazi na ufanisi pamoja na kuwafanya wananchi kupata taarifa mbali mbali za serikali.
Blogu hii inaipongeza idara eGA kwa kazi kubwa iliyofanya na inayofanya ya kuwezesha serikali kutoa huduma kwa haraka na ufanisi mkubwa kupitia matumizi ya mtandao wa Internet nchini. Blogu hii inaomba juhudi hizi ziendelezwe ili kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi iliyopiga hatua katika matumizi ya TEHAMA duniani. Kwa taarifa zaidi bonyeza
hapa

Picha:
http://www.ega.go.tz/
No comments:
Post a Comment