Hongera Halmashauri ya Kinondoni kwa kuhamisha kituo cha daladala cha Mwenge na kukipeleka Makumbusho. Aidha blogu hii inaipongeza Halmashauri kwa kutoa sababu ya kuhamisha na kubomoa kituo hicho. Sababu kuu ni kupisha upanuza wa barabara ya Morocco kwenda Mwenge (sababu hii ni ya msingi), sababu ya pili ni kuboresha usafi (ni ya msingi pia). Blogu hii inashauri Halamashauri kujenga barabara za lami kwa njia zote zinazoingia na kutoka kituo kipya cha makumbusho. Njia za sasa sio za lami na hii itasababisha barabara kuchimbika sana kutokana na magari makubwa (mabasi) kupita njia hizo zisizo na lami na kusababisha usumbufu hasa wakati wa mvua. Pia blogu hii inashauri uwezekano wa kupanua kituo cha Makumbusho kwa kubomoa sehemu ya soko. Kwa mtazamo wa blogu hii kituo ni kidogo. Pia utaratibu wa kituo ubadilishwe kwa maana mabasi yakae kituoni si kwa zaidi ya dakika 5 (yaani yaingie na kutoka SIO kukaa muda mrefu ili kujaza abiria).
Pia blogu hii inaomba suala la USAFI lizingatiwe KIKAMILIFU katika KITUO kipya cha MAKUMBUSHO.
- Halmashauri iweke utaratibu wa kukisafisha muda wote kituo hiki (ikiwezekana kampuni ipewe zabuni ya usafi);
- Kuwepo na huduma za vyoo;
- Kuwepo na sehemu nyingi za kutupa takataka (siyo kila sehemu ni jalala);
- Kuwepo na faini kwa mtu yoyote atakaye tupa takataka ama uchafu wa aina yoyote;
- Ikiwezekana kuwe na mahakama ya papo kwa papo.

Picha:http://dewjiblog.com/ - sehemu ya kituo cha daladala cha mwenge baada ya kuzuiwa
No comments:
Post a Comment