
Picha:
Hongera sana Mh Leticia Nyerere
kwa kuwa mzalendo. Hakika blogu hii imefurahishwa sana kwa jinsi alivyokuwa
akichangia hoja ya kuridhia itifaki ya SADC
fedha na uwekezaji katika bunge la
bajeti linalofanyika Dodoma, Tanzania tarehe 06/06/2014. Mh Leticia amesikitishwa na jinsi
watanzania wasivyo wazalendo, wanaoshabikia masuala ya ajabu ajabu.
Amesikitishwa jinsi watanzania wasivyojivunia nchi yao na kuipenda. Ameshauri
serikali iwaandae watanzania kushiriki katika jumuia hizi kama SADC na sio
kuridhia tu. Watendaji wa serikali pamoja na watanzania wakiandaliwa vyema
watakuwa washiriki wazuri katika SADC na kukuza uchumi wa nchi yetu. Pia
watendaji wakiwa wazalendo nchi yetu itapata manufaa makubwa sana. Mh Leticia
amesema watanzania wakiandaliwa na kushirikishwa kikamilifu, taifa litapiga
hatua kubwa ya maendelo. Kwa kuridhia ya SADC
fedha na uwekezaji, Tanzania itaweza
kushirikiana na nchi nyingine katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Tuwe WAZALENDO, ili tupige hatua
kubwa ya maendeleo. Asante sana Mh Leticia Nyerere kwa kuwa mzalendo.
Hakika, blogu hii imekumbushwa maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere miaka ya 60, “binadamu wote ni sawa na Afrika ni MOJA”
No comments:
Post a Comment