MATENGENEZO ya uwanja mpya na wa kisasa wa klabu ya Simba kama ilivyoahidiwa na uongozi unaomaliza muda wake chini yake Alhaj Ismail Aden Rage umeanza (Picha:)
Hongera sana uongozi wa Simba Sports Club unaomaliza muda wake kwa mambo makubwa yaliyofanyika na yanayofanyika sasa chini ya Mh Rage. Kwa baaadhi ya watanzania wataona mambo haya ni madogo na wengine wataanza yale maneno yetu "Kwanini hawakuanza zamani?? Kwanini sasa?? nk" Maswali haya, siyo ya msingi, maana uongozi wa Simba unaomaliza muda wake umetimiza ahadi kwa wanachama wao nao ni kujenga uwanja wa mazoezi.
Blogu hii inaomba kuwaeleza wadau wake kuwa kujenga uwanja sio jambo dogo. Mafanikio ya UONGOZI wa Mh Rage katika hili ni:
- Kutafuta eneo la uwanja (limepatikana Bunju);
- Kujenga uwanja wa mazoezi katika eneo hilo (kazi inaendelea ya kuondoa udongo wa asili na kuweka nyasi zinazotakiwa-kazi inaendelea);
- Kuweka maandalizi ya kujenga hostel pale Bunju;
- Kuweka maandalizi ya uwanja wa kisasa (hiyo ni kazi ya viongozi watakaokuja baada ya Uchaguzi mwezi huu wa sita, 2014).
Blogu hii kwa makusudi kabisa inaupongeza uongozi unaomaliza muda wake chini ya mpiganaji asiyechoka Mh. Alhaji Ismail Aden Rage. Uongozi wa Mh Rage ndani ya Simba ulikabiliwa na upinzani usiokuwa na tija ambao ulisababisha baadhi ya mambo kutofanyika vizuri ama kwenda kinyume. Lakini bado blogu hii itamkumbuka sana Mh Rage na hasa kwa hili la kuwaachia wanamsimbazi UWANJA wa MAZOEZI ambao watakaokuja watajenga UWANJA mwingine MKUBWA pamoja na majengo ya hostel, ofisi nk. Hongera Mh Rage kwa kawaida mtu hathaminiwi kwao ila wachache tunatambua mchango wako. Hongera.
Ushauri kwa watani wa SIMBA yaani YANGA nao wafikirie kwenda Bunju ama Kisarawe ama kokote kule nje ya mji wa Dar es Salaam watakapopata eneo kubwa kama SIMBA walivyofanya ili kujenga "Complex ya michezo" yenye hosteli, ofisi, maduka ya vifaa vya michezo kama jezi, mahotel, sehemu ya kuogelea pamoja na UWANJA mkubwa wa kisasa.
Picha: 24tanzania.com
No comments:
Post a Comment