Hongera sana Mh Ummy Mwalimu kwa
kutilia mkazo upandaji wa miti nchini. Mh Ummy ameshiriki katika upandaji miti
Same mkoani Kilimanjaro katika kijiji cha Mabilioni tarehe 17/06/2014 ikiwa ni
siku ya kupambana na hali ya jangwa na ukame duniani.
Upandaji miti una faida nyingi
ikiwa ni pamoja na utunzaji mazingira ambapo kwa sasa ni suala la kimataifa.
Upandaji wa miti pia unapendezesha manthari ya sehemu husika. Na mwisho miti
huongeza pato la taifa kwa maana ya uvunaji na uuzaji wa mazao yatokanayo na
miti kama mbao. Pia blogu hii imefurahishwa na mkakati wa kuhakikisha Halmashauri
nchini zinatilia mkazo suala la upandaji miti. Pia blogu hii imefurahishwa suala la
kuhamasisha makundi hasa ya vijana katika suala zima la upandaji miti.
Blogu hii inaomba licha ya juhudi
za kupanda miti nchini pia kuwe na sheria na kanuni za kukata miti. Kuwa na
utaratibu huu utaokoa miti mingi inayokatwa bila sababu ya msingi na hivyo
kuharibu mazingira. Ipo mifano mingi ya watu kukata miti bila sababu za msingi.
Kuwepo kwa sheria na kanuni kutawabana wale wote wanaofikiria kuharibu
mazingira kwa kukata miti hovyo. Tanzania inaweza kuwa na sheria ama kanuni ya
kama mtu ama kikundi kikitaka kukata mti lazima kiombe kibali (tunaweza kuanzia
katika ofisi za mtaa/kijiji) ambazo zinatambuliwa na Halmashauri. Ni vizuri
kukumbushana katika nchi zilizoendelea sio rahisi kukata mti ovyo LAZIMA uombe
kibali toka mamlaka husika, hivyo Tanzania tuige mfano huo.
Blogu hii inaomba wadau wengine
wa mazingira wamuunge mkono Mh Ummy katika jitihada za kupanda miti na kutunza
mazingira.

Mh Ummy Mwalimu akipanda mti, katika kijiji cha Mabilioni, Same mkoani Kilimanjaro tarehe 17/06/2014
No comments:
Post a Comment