Monday, June 9, 2014

Hongera sana Neema Loy kwa kuanzisha blogu ya "Hayana Tuinuke"

Picha Yangu
Picha: http://neemaloy.blogspot.com/ - Neema Loy

Hongera sana Neema Loy kwa kuanzisha blogu ya "Hayana Tuinuke" . Madhumuni ya blogu uliyoianzisha ni kwaajili ya mambo mbalimbali kama vile mambo ya kielimu, kisiasa, kiuchumina mengineyo. Hakika kama mdau na mmiliki wa blogu "tuijenge tanzania" nimefurahishwa sana na jinsi ulivyovikilia na kunzisha blogu ya namna hii. Ni imani yetu kuwa blogu uliyoianzisha itakuwa taa kwa vijana wenzako katika kujiletea maendeleo. 


Licha ya kutoa habari kwa watu mbalimbali lakini blogu ni uchumi ukiangalia kwa jicho la tatu. Sina maana ya kupata pesa kupitia matangazo (kama blogu zingine zinavyofanya) ila jinsi watu wengi watakavyotembelea blogu husika basi yenyewe inapata umaarufu ambao unakuunganisha na fursa ambazo kwa sasa utaona kama ndoto. Karibu kwenye fani hii.

3 comments:

  1. Asante sana lecturer wangu, unanitia moyo kwani mwanzo ni mgumu siku zote na wajanja tu ndio wanaoweza kujua na kusapoti siri hii!

    ReplyDelete
  2. Asante sana Neema, unajua watu wengi hawajui umuhimu wa vitu hivi. Dunia ishakuwa kama kijiji kidogo sana kwa hiyo ukitumia fursa hii sio lazima wale waliokuzunguka ndio utafaidika nao bali hata watu wa mbali sana ambao hutatarajia ndio utaungana nao kwa mambo mengi yenye faida zisizo hesabika kwa maneno the limit is sky. Mimi kutembea sehemu nying duniani mojawapo ni kuwa na vitu kama hivi, kwa tecknolojia ya leo kuwa na vitu hivi kama blogs na mitandao mingine ni sawa na kuwa na shamba, gari ama mali kama watu wazamani walivyokuwa navyo. utashangaa hata gari nachukulia ni mali za zamani. Natamani siku moja niwaelimishe watu makini umuhimu wa vitu hivi na namna gani wanapaswa kufanya

    ReplyDelete