Picha: mapsofworld.com
Hongera kwa serikali pamoja na jamii nzima ya Tanzania kwa ongezeko la UMRI wa KUISHI hapa TANZANIA. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, umri wa kuishi kwa watanzania umeongezeka kutoka miaka 50 (sensa ya mwaka 1988) hadi kufikia miaka 61 (sensa ya mwaka 2012).
Hayo yalisemwa na mkurugenzi mkuu wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk Albina Chuwa wakati akiwasilisha taarifa za
msingi za kidemografia, kijamii na kiuchumi kwenye hafla ya uzinduzi
iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Aidha, alisema wanawake wanaishi umri
mrefu zaidi kuliko wanaume. Matokeo haya yanaonyesha wastani wa umri wa
kuishi kwa wanawake ni miaka 63 tofauti na wanaume ambao ni miaka 60.
Ongezeko la umri wa kuishi limetokana na
kukua kwa uchumi na kupungua kwa umaskini wa kipato miongoni mwa wananchi wa
Tanzania. Aidha pia ongezeko hili linatokana na juhudi za serikali katika
kuwaletea wananchi wake maendeleo na kutoa huduma za kijamii kama afya, elimu
nk.
Blogu hii inaomba juhudi hizi ziimarishwe
na serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo wa nchi hii ili umri angalao
ufikie miaka 70 ya kuishi. Wadau wa maendeleo sio tu wale wanaotoa msaada
mikubwa kwa taifa letu BALI hata yale mashirika yasiyo ya kiserikali nchini,
taasisi na makampuni ya watu binafsi (mfano kuna hospitali na shule binafsi)
nk.
Kwa habari zaidi soma mwananchi.
No comments:
Post a Comment