Tuesday, July 30, 2013

Uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kyaka - Bugene mkoani Kagera uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete

Uzinduzi wa ujenzi wa barabara za mikoani hasa mikoa ya pembezoni ni jambo linalochochea maendeleo ya taifa. Blogu hii inatoa pongezi kwa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kyaka mpaka Bugene uliofanyika Bunazi mkoani Kagera na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete. Mbali na kuipongeza serikali kwa juhudi hizi pia blogu hii inapenda kuomba barabara zingine zizidi kujengwa.

Aidha blogu hii inaiomba serikali kuwa na mikakati endelevu ya kuzuia uharibifu wa barabara zinazojengwa kwa gharama kubwa. Kuwepo na faini kubwa na kali kwa wale wote wanaokiuka sheria katika utunzaji na utumiaji bora wa barabara hasa za kiwango cha lami na changarawe.

Picha hii ni kutoka DailyNews Online Edition.











Monday, July 29, 2013

Hongera AZAM kwa kupanga kurusha matangazo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara

Hongera SSB kampuni ya AZAM kwa kupanga kurusha matangazo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Hatua hii ni ya kujivunia si tu kwa vilabu bali pia kwa wapenzi wote wa soka ndani na nje ya Tanzania. Moja ya faida ya kufanya hivi ni wachezaji kupata soko la kimataifa na baadhi ya klabu ndogo kupata mapato ya kuendesha klabu zao. Kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) ambayo inayomiliki klabu ya Azam FC itatenga 1.5 bilioni kwa timu zote za ligi kuu Bara msimu ujao ili kurusha moja kwa moja matangazo kupitia televisheni iitwayo AZAM TV. Kwa habari zaidi wasiliana na kitongojini



Picha:http: kitongoni.blogspot.com

Thursday, July 25, 2013

Hongera Mkuu wa wilaya ya Iramba Mh. Nawanda kwa kuhamasisha wananchi juu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji

Hongera sana Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida Mh. Yahaya Nawanda kwa kuanzisha mradi wa kuku wa kienyeji wanaokadiriwa kufikia 966 na kuwahamasisha wananchi ili nao waweze kuiga mfano wako huo. Hakika hatua hii ni ya kuungwa mkono sio na viongozi wenzako bali hata wananchi kwa ujumla. Pia tunapongeza na kuthamini juhudi zako za kuongoza kwa vitendo. Hakika unatukumbusha enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyependa kuongoza kwa vitendo. Baba wa taifa licha ya kuhimiza kilimo alikuwa ni mkulima ambaye wakati alipopata wasaa alikwenda shambani bila ya kujali cheo na hadhi yake kubwa nchini. Blogu hii inakupongeza na inaomba viongozi wengine waige mfano huu. Pia kwa wananchi mmoja mmoja ni wakati muafaka kuiga namna Mh Nawanda afanyavyo.  Na kwa kufanya hivi umaskini utakuwa historia pamoja na kuondoa kabisa magonjwa ya utapiamlo kwa watoto nchini. Kwa taarifa kamili na picha mbalimbali za tukio hili tembelea dewjiblog.


DSC02244-02244 
Chanzo: http://dewjiblog.com



Tuesday, July 23, 2013

HONGERA Mh. Jerry Silaa kwa ujenzi wa kivuko cha miguu kwenda ulongoni

Kwa mujibu wa Jerry Silaa ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto amesema ujenzi wa kivuko cha miguu kwenda ulongoni kuanza punde kwa ufadhili wa diwani wa kata ya Gmboto. Hakika msomaji unaweza kuona kama jambo hili ni dogo lakini lina manufaa makubwa kwa jamii yetu. Kama madiwani wote nchini wakifanya juhudi kama hii kwa hakika nchi yetu itapiga hatua kubwa ya maendeleo. Blogu hii inatambua mchango wako na pia inakuomba uzidi kuiletea maendeleo kata yako na manispaa kwa ujumla.

Kwa kuwa shabaha ya blogu hii ni pamoja na mambo mengine kupongeza juhudi za maendeleo zinazofanywa na watanzania kwa ajili ya watanzania na kwa kutambua mchango wako blogu hii ingependa wananchi wajue huyu Mh Jerry ni nani? Fungua hapa


 
  Chanzo: Mh. Jerry Silaa