BUSARA toka kwa Mkubwa Kambi - TAIFA Stars isikate tamaa! CHAN twaweza kwenda!!
Mwanzo wa nukuu toka kwa Mkubwa Kambi
"Kwa
wale wapenzi wa soka someni kwa makini mkasa huu,1983 Waganda hawa hawa
walitufanya mbaya pale National Stadium walitupiga kidude katika
pambano la kwanza, washabiki walishikwa na hasira kweli wachezaji
iliwalazimu kutoka uwanjani saa tatu usiku, kwenye kichwa cha habari cha
gazeti la mfanyakazi James Nhende aliandi, "Mogela afunikwa" pamoja na
kebehi kibao kutoka kwa mashabiki, Zamoyoni Mogella alimpiga mwandishi
yule na file likafunguliwa polisi.
Baada ya siku mbili tatu Charles
Bonface "Mkwasa", Zamoyoni Mogella, Lilla Shomari wakatangaza kujiuzulu
kuchezea Stars, FAT (TFF) nayo na serikali waliona hakuna haja tena timu
ya Taifa kwenda kucheza mechi ya marudiano kule Uganda kwani ilikuwa ni
gharama (ikumbukwe enzi zile hakuna udhamini).
Baadhi ya wadau wa
soka walijaribu kuzungumza na wachezaji tatizo lilikuwa nini, nao
waliitaja moja ya sababu ni upangaji wa timu, wakati huo ilikuwa chini
ya Kocha Geff Hudson (muingereza).
Wachezaji wakaketishwa
chini pamoja na kocha wao wakafikia muafaka, serikali ikaombwa
igharamie usafiri vijana waende Uganda na wale wachezaji waliotishia
kujiuzulu walirudi kundini. Vijana wale wakapatiwa ATC wakaenda zao
Uganda na kikosi cha timu walikipanga wenyewe kocha akiwa msimamizi tu,
ndani ya dakika 15 Uganda ameshapigwa goli mbili za Zamoyoni Mogella,
Celestine "Sikinde" Mbunga akashindilia msumari wa mwisho, hadi mwisho
Sisi 3 wao 1 tukasonga mbele.
Kwenye soka hakuna
lisilowezekana, tatizo la wachezaji wetu wa kizazi hiki wamekosa
kujiamini hivyo kushindwa kuongea hata kama tatizo wanaliona, nafasi
naamini bado tunayo tujipange tuache mipango ya zima moto wiki mbili
zinatosha kumuua mganda.
Kila la heri Taifa Stars, jitambueni."
Mwisho wa nukuu toka kwa Mkubwa Kambi
No comments:
Post a Comment