Hongera sana Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa
wa Singida Mh. Yahaya Nawanda kwa kuanzisha mradi wa kuku wa kienyeji wanaokadiriwa kufikia 966 na kuwahamasisha wananchi ili nao waweze kuiga mfano wako huo. Hakika hatua hii ni ya kuungwa mkono sio na viongozi wenzako bali hata wananchi kwa ujumla. Pia tunapongeza na kuthamini juhudi zako za kuongoza kwa vitendo. Hakika unatukumbusha enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyependa kuongoza kwa vitendo. Baba wa taifa licha ya kuhimiza kilimo alikuwa ni mkulima ambaye wakati alipopata wasaa alikwenda shambani bila ya kujali cheo na hadhi yake kubwa nchini. Blogu hii inakupongeza na inaomba viongozi wengine waige mfano huu. Pia kwa wananchi mmoja mmoja ni wakati muafaka kuiga namna Mh Nawanda afanyavyo. Na kwa kufanya hivi umaskini utakuwa historia pamoja na kuondoa kabisa magonjwa ya utapiamlo kwa watoto nchini. Kwa taarifa kamili na picha mbalimbali za tukio hili tembelea dewjiblog.
Chanzo: http://dewjiblog.com
No comments:
Post a Comment