Monday, July 22, 2013

Watanzania tuenzi utalii wa ndani ili kuongeza pato la taifa

Kwa hakika nchi yetu imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii. Nchi hii ina misitu, mbuga za wanyama, milima na mabonde ya kuvutia. Kwa uchache vipo vitu vingi vizuri nchini Tanzania. Kwa leo napenda kuwahamasisha watanzania wenzangu kutembelea maeneo ya utalii kama ifuatavyo:

  1. Msitu wa Ugalla
  2. Mbuga ya Mahale
  3. Gombe
  4. Mlima wa Udzungwa
  5. Mbuga ya Ruaha
  6. Mbuga ya Mikumi
  7. Mbuga ya Saadani
  8. Manyara
  9. Tarangire
  10. Arusha
  11. Kilwa kisiwani
  12. Mlima Kilimanjaro
  13. Ziwa Victoria
  14. Mbuga ya Serengeti
  15. Kisiwa cha Mafia
  16. Ngorongoro
  17. Vivutio vya utalii mkoa wa Lindi
  18. Selous
  19. Zanzibar na Pemba
  20. Olduvai
  21. Bagamoyo
Hakika machozi ya furaha yaweza kukutoka, maana vivutio hivi ni baadhi tu. Naomba tuwe sehemu ya utalii wa ndani katika nchi yetu.


Tuchangamkie utalii wa ndani. Napenda kutoa wito kwa mashule, vyuo, idara za serikali, mashirika ya umma na watu binafsi pamoja na wananchi kwa ujumla kuwa na utaratibu na utamaduni wa kutembelea vivutio vya kitalii hapa nchini. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeenzi vivutio vyetu na kuongeza pato la taifa kupitia utallii wa ndani.

No comments:

Post a Comment