Blogu hii ni kwa ajili ya kuonyesha, kupongeza na kuhamasisha juhudi ama mambo yoyote ya kimaendeleo yanayofanyika ndani na nje ya Tanzania kwa faida ya watanzania wote.
Monday, July 15, 2013
Hongera Mh. Mwakyembe kwa ongezeko la pato la bandari toka Tshs 28 bilioni mpaka Tshs 50 bilioni kwa mwezi
Hongera Mh. Harrison Mwakyembe kwa kufanikisha ongezeka la pato la bandari toka Tshs 28 bilioni kwa mwezi mpaka kufikia Tshs 50 bilioni. Hakika mafanikio haya mbali na kuisaidia mamlaka yenyewe ya bandari kuongeza mapato pia fedha hizi zinaingia kwenye uchumi wa Taifa letu changa. Ukiangalia ongezeko hilo ni kama asilimia mia moja. Fedha hizi ndizo zinazoleta maendeleo kama vile ujenzi wa barabara za lami, kulipa huduma za jamii n.k. Watanzania tunaamini pato hili laweza kuongezeka zaidi kwa serikali kuzidi kuliboresha shirika letu hilo. Hakika Tanzania tunajifunia kuwa na viongozi wa staili hii (Results oriented). Kwa taarifa kamili wasiliana na mwananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment