Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete jana jumapili alifungua Tamasha la MATUMAINI nchini Tanzania. Binafsi uwepo wa TAMASHA la namna hii ni jambo jema sana maana linahamasisha amani na kuaminiana miongoni mwa wanajamii na pia linaunganisha wananchi na wawakilishi wao. Binafsi naomba juhudi hizi ziendelezwe kwa ustawi wa taifa letu.
Katika tamasha hilo, miongoni mwa mambo mengine Timu ya Wabunge wa YANGA iliwafunga wenzao wa SIMBA. Kwa walioshinda, HONGERA SANA, na timu iliyoshindwa IJIPANGE kwa ajili ya TAMASHA lingine maana nao walijitahidi sana.
Unaweza tembelea blogu page ya
Jane John au
Shaffih Dauda kwa kuangalia picha mbali mbali.

Picha: http://janejohn5.blogspot.com
No comments:
Post a Comment