Saturday, July 8, 2017

Hongera timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" kwa kuchukua nafasi ya 3 ya COSAFA

Tokeo la picha la tanzania flag
Picha: wikipedia

Hongera timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" kwa kushika nafasi ya 3 ya mashindano ya COSAFA nchini Afrika Kusini. Ushindi huo umekuja baada ya kuifunga Lesotho kwa mikwaju ya penati. Hakika wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa TFF chini ya Rais Jamal Malinzi mnastahili pongezi kwa hatua hii. Kipekee blogu hii inampongeza kocha Salum MAYANGA kwa kuiboresha timu ya Tanzania. Hakika, hivi sasa Tanzania inacheza soka zuri na la ushindani ukilinganisha na miaka ya nyuma. Hatua hii itainua Tanzania katika viwango wa FIFA na pia wachezaji watapata soko kimataifa. Aidha hatua hii imewafanya wachezaji kupata uzoefu na kuzoeana na hii itaiwezesha Tanzania kufanya vizuri katika michuano mingine ya kimataifa. 

Monday, June 12, 2017

Big UP kamati ya Profesa Osoro, "Raslimali za MADINI zitamkwe kuwa MALI ya WATANZANIA"

Tokeo la picha la Nehemiah Eliachim Osoro

Hongera kamati ya pili ya MAKINIKIA iliyoteuliwa na Mh Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa kuja na uchambuzi wa kina wa kiuchumi na kisheria. Kamati hii ya PILI chini ya uenyekiti wa Profesa Nehemiah Eliachim Osoro imefanya kazi nzuri kwa maslahi mapana ya taifa. Blogu hii inasema ASANTE. 

Blogu hii imefurahishwa na mapendekezo yote ya kamati ya PILI hasa "raslimali za MADINI zitamkwe kuwa MALI ya WATANZANIA".

Tokeo la picha la magufuli

Aidha blogu hii inampongeza Mh Rais kwa udhubutu wa kuamua masuala magumu ya kitaifa kwa maslahi ya taifa. Hakika, sasa Tanzania tunajivunia kuwa na kiongozi mtetezi na mlinzi wa raslimali zetu. Blogu hii inamuomba Mh Rais nguvu hii pia iende kwenye masuala mengine muhimu kama vile misitu, utalii, mikataba ya umeme, mikataba ya matumizi ya maji kwa ziwa Victoria nk ili watanzania wanufaike.

Tokeo la picha la KAMATI YA PILI YA MADINI WIKEPEDIA

 Picha: tanzaniatoday

Blogu hii inawaomba watanzania kuwa kitu kimoja katika harakati hizi za kutetea maslahi ya watanzania. Blogu hii inafahamu kuna kasoro ambazo zilijitokeza huko nyuma na kwa sasa serikali ya John Pombe MAGUFULI imedhamiria kuzifanyia kazi kikamilifu. Aidha blogu hii imefurahishwa na kauli ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Job Ndugai kwa kauli aliyoitoa ya kusaidiana na serikali kuzipitia na kurekebisha sheria za madini kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu. Blogu hii inasema ASANTE.


Tokeo la picha la job ndugai
Picha:ccm blog

Tuesday, June 6, 2017

Hongera Kamanda SIRRO kwa kuteuliwa kuwa IGP

Image may contain: 4 people, people smiling, people standing and outdoor
Hongera Kamanda SIRRO kwa kuteuliwa kuwa IGP. Hakika unastahili nafasi hii kutokana na utendaji wako na hasa ulipokuwa kamanda wa mkoa wa Dar es Salaam. Blogu hii inakuomba uchape kazi ili nchi iwe na amani na usalama zaidi. Aidha blogu hii inampongeza rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania DKT John Pombe Magufuli kwa kumteua kamanda SIRRO mchapakazi. 

Hongera mama Anna Mghwira kwa kuchaguliwa na rais kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro

Image may contain: 8 people, people smiling, people standing and suit

Hongera mama Anna Mghwira kwa kuchaguliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKT John Pombe Magufuli. Blogu hii inakutakia kila la kheri katika utendaji wako mpya wa Ukuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Ingizo lako katika serikali ni shule kwa watanzania wote, wenye vyama na wasio na vyama. Blogu hii inakuomba uwe mfano katika uwajibikaji kwa rais na kwa wananchi, hasa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro, uwe mwadilifu, mchapakazi na mtetea usawa kwa wote na hasa kwa kina mama na wanawake ambao bado katika nchi za kiafrika wanakabiliwa na changamoto nyingi. Aidha blogu hii inampongeza sana Mh Rais kwa uamuzi wake wa kumwamini mama ANNA ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa chama cha upinzani ACT Wazalendo. 

Wednesday, May 24, 2017

Hongera Rais MAGUFULI kwa kutetea rasilimali za Tanzania kupitia sekta ya madini

Tokeo la picha la magufuli
Picha: wikipedia

Hongera Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa kutetea rasilimali za Tanzania kupitia sekta ya madini. Blogu hii imefurahishwa na uamuzi wako wa kuteua Kamati Maalum ya kuchunguza mchanga wa mabaki ya madini ya dhahabu yanayosafirishwa nje ya nchi kupitia makontena. 

Kamati hiyo iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Profesa Abdukarim Hamis Mruma imefanya kazi nzuri kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Pia blogu hii inakupongeza kwa uamuzi wako wa leo wa kuwawajibisha wahusika na kuvunja bodi ya TMAA. Kwa mujibu wa ripoti inaonekana taifa letu linapoteza mapato makubwa kutokana na tofauti ya kiasi cha madini kinachosafirishwa kupitia makontena ya mabaki ya dhahabu na madini mengine.

Image may contain: 1 person, sitting

Aidha, blogu hii inaomba yafuatayo:
  • Watendaji wa serikali pamoja na taasisi zake ziwe makini na kufuatilia kwa karibu thamani halisi ya madini yanayochimbwa na pia kusafirishwa nje kupitia mchanga wa madini au madini halisi;
  • Ni vizuri taasisi kama TMAA, TRA, TBS na mamlaka za Bandari na viwanja vya ndege wafuatilie kwa umakini kiasi halisi cha madini kinachotoka nje ya nchi na kila taasisi ikiwezekana iwe na kumbukumbu zake;
  • Pia kuwepo na vifaa vya kiteknolojia vya kuchunguza kwa umakini makontena au mizigo inayopita bandarini na viwanja vya ndege;
  • Vyombo vya ulinzi na usalama vishiriki kikamilifu kulinda rasilimali za taifa na hasa kupitia katika mipaka ya nchi yetu;
  • Suala la MAADILI litiliwe mkazo kwa watumishi wote wa umma;
  • Taifa kupitia Wizara ya Nishati na Madini linunue kifaa cha kuchenjua madini "smelter" ili taifa liweze kupata faida ya rasilimali ya madini kwa uhalisia wake.

Kila la kheri Mh Rais Magufuli katika kulinda rasilimali za taifa. Watanzania tupo nyuma yako!

Sunday, May 21, 2017

Hongera Faidha Msangi kwa kushinda Urais wa Serikali ya Wanafunzi wa IAE

Tokeo la picha la institute of adult education
Hongera Faidha Msangi kwa kushinda Urais wa Serikali ya Wanafunzi wa Institute of Adult Education (IAE) mei 2017. Blogu hii imefurahishwa na ushindi wako ukiwa kama mwanamke shupavu. Ushindi wako umewaamsha wanawake na wanaume kuwa siku hizi na siku zijazo kuna fursa ya kila mwanamke na mwanamme kushinda ngazi yoyote ya uchaguzi bila tatizo lolote. 


Image may contain: 3 people, closeup
Uchaguzi huu unaweza kuonekana ni mdogo katika nchi yetu ila unatoa somo la kujifunza kwa jamii yetu ambayo imeathiriwa na mfumo dume. Blogu hii inaamini maendeleo ya kweli katika taasisi na jamii yoyote yatapatikana kwa kutoa nafasi sawa kwa wanawake na wanaume bila ubaguzi. 

Tokeo la picha la institute of adult education

Blogu hii inakuomba utumikie nafasi yako kwa weledi, ustadi na nguvu za hali ya juu ili jamii yetu izidi kupata imani kuwa mwanawake na mwanaume anaweza uongozi bila kujali jinsi. 


Blogu hii inaamini kama mwanamke anaweza kulea mtoto mpaka anakuwa mtu mzima basi bila shaka uwezo wa kuongoza taasisi au jamii upo ndani yake pia. Kila la kheri Faidha Msangi. Hakika wanawake WANAWEZA!

Sunday, May 14, 2017

Asante Mh Nyarandu, Samaritan's Purse na Serikali kwa kusaidia kuwapeleka watoto walionusurika na ajali Marekani kwa matibabu zaidi

Image may contain: 13 people, crowd, wedding and outdoor
Kwa hili la kusaidia kupeleka watoto watatu Marekani kwa ajili ya matibabu ni jambo la kupongezwa. Mh Lazaro Nyarandu, Mbunge wa Singida Kaskazini, Shirika la Kujitolea la Marekani Samaritan's Purse na Serikali ya Tanzania kwa hili mnastahili pongezi za dhati kabisa. 

No automatic alt text available.
Watoto hawa ni majeruhi wa ajali iliyopoteza uhai wa watoto, walimu na dereva wa shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha. Takribani zaidi ya watu thelathini walipoteza maisha wengi wao wakiwa wanafunzi wa darasa la saba waliokuwa wakielekea Karatu toka Arusha kwa ajili ya mitihani ya ujirani. 

Image may contain: outdoor
Blogu hii pia inawashukuru wafadhili (Samaritan's Purse) wa safari hii ya kwenda nchini marekani kwa matibabu zaidi. Aidha blogu hii inaishukuru Serikali ya Tanzania katika kufanikisha hili na kwa kukubali watoto hawa waende nje kwa matibabu zaidi.

Image may contain: sky, cloud and outdoor

Saturday, May 13, 2017

Hongera Sir Tenga kwa kuteuliwa kuwa Rais wa Kamati ya Usimamizi wa Leseni za Klabu, CAF

Tokeo la picha la leodegar tenga
Hongera Sir Leodegar Tenga kwa kuteuliwa kuwa Rais wa Kamati ya Usimamizi wa Leseni za Klabu, katika Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Afrika (CAF). Hakika unastahili kushika nafasi hii. Blogu hii inatambua heshima na weledi wako tangu ulipokuwa Rais wa heshima wa TFF. Blogu hii inakuomba kutumia uzoefu wako katika nafasi uliyopata kuisaidia Tanzania katika soka na hasa katika ushauri kwa klabu zetu nchini. 
Tokeo la picha la CAF 

Kila la kheri Serengeti Boys kwenye mashindano ya Afrika chini ya miaka 17 nchini Gabon

Tokeo la picha la serenget boys
Kila la kheri Serengeti Boys kwenye mashindano ya Afrika chini ya miaka 17 nchini Gabon. Blogu hii imefarijika sana na maandalizi chini ya Rais wa TFF Jamal Malinzi na benchi la ufundi. Aidha watanzania wana matumaini makubwa kutokana na mechi za majaribio za timu hii ilizocheza. Watanzania tupo nyuma yenu.
Tokeo la picha la CAF

Tuesday, May 9, 2017

Hongera Mh Ummy Mwalimu kwa kuwajali wazee wetu


Tuwaenzi wazee wetu. Hongera Mh Ummy Mwalimu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kuwakumbuka wazee wetu hasa waliopigania taifa letu. Blogu hii imejisikia faraja baada ya kuona ukiwa na Mama Maria Nyerere. Mama Maria ni mmoja wa wazee wetu mashuhuri. Blogu hii inaomba ukiwa kama Waziri unayeshughulikia pia masuala ya wazee uendelee kuwapa kipaumbele wazee wetu hasa katika masuala ya afya na matibabu kisera na kimkakati. Blogu hii inatambua kuwa wazee wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo maradhi yanayotokana na umri mkubwa.

Monday, May 8, 2017

Hongera viongozi wapya wa Tanzania Australia Alumni Association (TAAA) kwa kuchaguliwa kuongoza chama hiki

Picha: Viongozi wakuu wa TAAA waliochaguliwa VETA Mikumi 6 Mei 2017. Kutoka kulia n
Rais ndugu Makassy, Makamu wa Rais Ms Mary Awinia, Katibu ndugu Bonface Kyaruzi 
na Naibu Katibu ndugu Sarah Dotto

Hongera viongozi wapya wa Tanzania Australia Alumni Association (TAAA) kwa kuchaguliwa kuongoza chama hiki juzi 6 Mei 2017 VETA Mikumi, Morogoro. TAAA ni chombo kinachoundwa na wanafunzi waliosoma nchini Australia.

Image may contain: grass, outdoor and nature
Picha: Wanyama ndani ya Mikumi National Park toka VETA Mikumi 7 Mei 2017

Lengo la TAAA ni kuwaunganisha pamoja wanafunzi waliosoma nchini Australia ili kuiletea Tanzania maendeleo ya kweli kupitia Elimu, Ujuzi na Maarifa toka nchini Australia. Viongozi wa TAAA waliochaguliwa ni Rais ndugu Charles Makassy, Makamu wa Rais ndugu Mary Awinia, Katibu ndugu Boniface Kyaruzi, Naibu Katibu ndugu Sarah Dotto na Mweka Hazina ndugu Nzamba. Aidha TAAA imepata wajumbe watano wa kamati ya utendaji nao ni ndugu Geofrey Felix Kalumuna, Boniphace Paul, Henry Mditi, Pamela Levira na Robert Mashinji.

Image may contain: 12 people, people standing, outdoor and nature
Picha: Viongozi wakuu wa TAAA pamoja na wajumbe watano wa kamati ya utendaji nje ya Mikumi National Park 7 Mei 2017

Blogu hii inaomba waliochaguliwa kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya TAAA na kuiletea Tanzania maendeleo ya kweli. Blogu hii inaamini kuwa viongozi na wanachama wa TAAA wana elimu, ujuzi na maarifa katika kuchochea maendeleo ya Tanzania kwa kasi.

Image may contain: one or more people, people sitting, table and indoor
Picha: wakati wa mkutano, VETA Mikumi, Morogoro Mei 6, 2017

Friday, May 5, 2017

Hongera Mh Ummy kwa ahadi ya kuunguza vifo vya wanawake wajawazito nchini

Image may contain: 1 person, sitting, table and indoor
Jana Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania lilipitisha bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa fedha 2017/18. Blogu hii inampongeza Waziri Mh Ummy Mwalimu kwa hotuba yake nzuri iliyowafanya wabunge wapitishe bajeti hiyo. Blogu hii inajua umuhimu wa huduma za afya nchini na hivyo ahadi zote zilizotolewa na kupangwa na Wizara zikitekelezwa kikamilifu hasa kuokoa vifo kwa wanawake wajawazito na watoto.
Image may contain: 4 people, outdoor
Blogu hii inafahamu kuwa Wizara hii ina mambo mengi sana ya kuyatekeleza kwa maana wa ukubwa na majukumu yake. Blogu hii inaomba watumishi na watendaji wa sekta ya afya na Wizara kwa ujumla kuimarisha huduma za afya nchini.

Aidha blogu hii inaomba serikali iweke na kutangaza utaratibu wa kutoa huduma kwa wazee hasa za afya na matibabu. Blogu hii inaamini kuwa kuna utaratibu wa kuwahudumia wazee lakini kuna haja kuwe na utaratibu wa kuwajulisha watanzania juu ya huduma fulani fulani kwa wazee kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Blogu hii inajua wazee hukosa nguvu na fedha za kujihudumia kiafya wakiwa na umri mkubwa.

Hongera Makamu wa Rais Mama Samia kwa kuwapa kipaumbele makandarasi wa ndani

Image may contain: 1 person, closeup
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakandarasi wa ndani jana (04 MEI 2017) amesema serikali itawapa kipaumbele wakandarasi wa ndani. Hakika tamko hili limekuja wakati muafaka ambapo itainua kipato cha wakandarasi wa ndani na kuinua uchumi wa nchi.

Blogu hii inaomba wakandarasi wa ndani wafanye mambo yafuatayo:
  • Kufanya kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa;
  • Kukamilisha kandarasi kwa viwango kwa mujibu wa mikataba;
  • Kukamilisha kandarasi kwa wakati na kwa mujibu wa mikataba;
  • Kujiunga pamoja na kushirikiana katika kazi ili kushindana na wakandarasi wa nje wenye nguvu.
Tokeo la picha la samia suluhu hassan

Aidha, blogu hii inaiomba serikali kuweka sera ambazo zitawawezesha makandarasi wa ndani kupata kiurahisi mikopo ya vifaa na kifedha.

Tuesday, May 2, 2017

Watanzania tutembelee MIKUMI ili kukuza utalii wa ndani


No automatic alt text available.
Watanzania tutembelee MIKUMI ili kukuza utalii wa ndani. Mikumi National Park ni mojawapo ya vivutio vizuri vya utalii Tanzania vyenye wanyama wengi wa porini. 

Image may contain: 1 person, standing and outdoor

Hivyo blogu hii inawahimiza watanzania watembelee mbuga hii kwa ajili ya kupunzika, kujifurahisha na kujifunza tabia mbalimbali za wanyama wa porini. Aidha blogu hii inaipongeza MIKUMI na TANAPA kwa ujumla kwa kuendeleza na kuimarisha utalii. 

Image may contain: outdoor and nature
Ni vyema MIKUMI na TANAPA kwa ujumla ikawahamasisha watanzania kutembelea mbuga zetu na kuinua pato la taifa. Blogu hii inaomba kufanyike maboresho hasa MIKUMI kwenye njia za mbugani hasa wakati wa vipindi vya mvua. 

Image may contain: grass, outdoor and nature
Blogu hii inajua mbuga za wanyama hazitakiwi ziwe na barabara za lami lakini wanaweza kuweka barabara za changarawe ili njia zipitike kwa urahisi na hasa kwenye vipindi vya mvua. Pia huduma za kulala na chakula ziimarishwe na ziwe kwenye viwango vya kimataifa ili kuwavutia watalii wa ndani na nje.  

Image may contain: sky, cloud, outdoor and nature

Hongera Mc Kinyemi kwa kuhamasisha wanawake katika ujasiriamali




Image may contain: 1 person, sunglasses
Hongera Mwajuma Kinyemi (Mc Kinyemi) kwa kuhamasisha wanawake katika ujasiriamali siku ya mei mosi. 

Image may contain: 1 person, table

Hakika blogu hii imefurahishwa sana kwa jinsi ulivyowahamasisha wanawake wenzako katika kujipatia kipato na kujijengea uwezo wa kiuchumi katika ngazi ya familia na taifa. 

Image may contain: 2 people, people sitting and hat

Blogu hii inaomba wanawake na wanaume wazidi kuwahamasisha wanawake wawezi kuwa wajasiriamali si wadogo tu bali kuwa pia wajasiriamali wakubwa na ikiwezekana kuwa na viwanda kuunga mkono kauli mbiu ya NCHI YA VIWANDA. 

Image may contain: 4 people

Blogu hii pia inawaomba watunga sera waweze kuwasaidia wanawake nchini kwa kuwa na sera nzuri za ujasiriamali kwa wanawake. Blogu hii pia inaomba suala la mafunzo kwa wanawake wajasiriamali litiliwe mkazo sana hasa kupitia kwenye vyuo vya ufundi (VETA) na Blogu hii inaamini kama mwanamke atakuwa na uwezo wa kiuchumi nchi yetu itasonga mbele na kuwa na maendeleo ya uhakika.

Monday, May 1, 2017

Hongera Mbao FC toka jijini Mwanza kwa kuingia FAINALI ya kombe la AZAM FA Cup

Tokeo la picha la mbao fc
Hongera Mbao FC toka jijini Mwanza (the rock city) kwa kuingia FAINALI ya kombe la AZAM FA Cup baada ya kuifunga timu kongwe ya YANGA ya jijini Dar es Salaam. Mbao FC imekuwa chachu kwa timu nyingine ndogo ukiondoa vilabu vya YANGA, SIMBA na AZAM. 
Tokeo la picha la mwanza

Blogu hii inaomba timu hii isibweteke na kuhakikisha inachukua kombe ili kuweka historia mpya nchini. Aidha vilabu vingine vidogo viige mfano wa Mbao FC. Blogu hii inaamini moja ya mafanikio ya Mbao ni kuwa na benchi zuri la ufundi, uongozi mzuri pamoja na wachezaji wenye vipaji na nidhamu ya mchezo. Ni muhimu kwa vilabu nchini Tanzania kuwa na vitu hivi muhimu kama Mbao FC. Hongera Mbao FC ya jijini Mwanza. 

Hongera Dr Fatma Hamad mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa la jinsia, DUCE

Image may contain: 1 person, standing
Hongera Dr Fatma Hamad mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa la jinsia "1st International Conference on Gender Issues in Higher Learning Institution". 
Image may contain: 3 people, people smiling
Hakika blogu hii inakupongeza kwa umahili na ustadi wako uliowezesha kongamano hili. Aidha blogu hii inawapongeza wajumbe wa kamati ya maandalizi wote pamoja na uongozi mzima wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam. 
Image may contain: 6 people, people sitting
Blogu hii inatarajia kuona makongamano mengine mengi katika chuo hiki yenye kuchochea maendeleo ya taaluma na nchi yetu. 
Image may contain: 12 people, people smiling, people standing
Blogu hii inaomba mapendekezo aliyoyatoa mgeni wa heshima Mh Ummy Mwalimu kwa niaba ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan yafanyiwe kazi, hasa suala la kufanya utafiti juu ya suala la elimu bure na ongezeko la wanafunzi wa kike na kiume nchini. 

Hongera DAS wa wilaya ya Nachingwea, Mh Husna Sekiboko kwa kuhimiza suala la usafi kwa vitendo

Image may contain: 1 person, standing, outdoor and nature
Hongera DAS wa wilaya ya Nachingwea, Mh Husna Sekiboko kwa kuhimiza suala la usafi kwa vitendo katika wilaya yako. Blogu hii imefurahishwa sana kwa jinsi unavyoongoza wilaya hii kwa vitendo. Blogu hii inapenda kukutia moyo na hamasa uendelee kuwatumikia watanzania kikamilifu. Blogu hii inaomba watendaji walio chini ya DAS huyu mchapakazi waweze kuweka utaratibu endelevu wa usafi. 

Image may contain: 1 person, standing, shoes, grass, outdoor and nature
Aidha blogu hii inawaomba viongozi wengine waige mfano mwema wa DAS wa Nachingwea, Mh Husna ili Tanzania iweze kupata maendeleo yanayostahili.

Image may contain: one or more people, people standing, grass, tree, shoes, outdoor and nature

Thursday, April 27, 2017

Hongera kampuni ya simu ya ZANTEL kwa kuwa Mdhamini Mkuu "Main Sponsor" kwenye kongamano la kimataifa la jinsia" DUCE

Image may contain: sky and outdoor
Hongera kampuni ya simu ya ZANTEL kwa kuwa Mdhamini Mkuu "Main Sponsor" kwenye kongamano la kimataifa la jinsia" DUCE 1st International Conference on Gender in Higher Learning Institutions" lililoandaliwa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (DUCE).  Madhumuni ya kongamano hili la kimataifa ni kuibua mambo mbalimbali yahusuyo jinsia kwa mtizamo wa taasisi za elimu ya juu katika kutetea usawa wa kijinsia na haki za kibinadamu.

Tokeo la picha la zantel
Blogu hii inawapongeza sana na kwa hakika ZANTEL ni mfano wa kuigwa nchini. Aidha huduma za ZANTEL ni nzuri sana na hasa kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini. Blogu hii inatoa wito wa wanafunzi wa Elimu ya Juu na wananchi wengine kwa jumla kujiunga na ZANTEL.